Mbarawa: Waliokopa nyumba za Serikali walipe haraka

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametoa mwezi mmoja kwa watu na taasisi zilizokopa nyumba za Serikali kulipa. Mbarawa aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Alisema anataka fedha hizo zilipwe haraka, vinginevyo atawataja katika vyombo vya habari watakaoshindwa kukamilisha madeni yao na kuagiza waondoke kwenye nyumba hizo. “Kama ni watu binafsi au taasisi za Serikali ni lazima walipe ili na sisi tuendelee kufanya kazi zetu vizuri.

Naomba mlisimamie hilo na fedha hizo zilipwe,” Mbarawa alisema. Aliongeza kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kasi inayostahili. Profesa Mbarawa alisema pia kuwa ufisadi katika wizara hiyo sasa ni mwiko. Alisema kuwa ufisadi hauangalii ukubwa wala udogo hivyo kwake uwe mdogo au mkubwa ni ufisadi tu.

“Ninajua na ninyi TBA mna kashfa zenu. Ninawaambia tutapambana na wajanja wajanja wote kwa sababu hatutaki tufike katika majipu,” alisema. Aidha, aliwataka wafanyakazi wa wakala huo kufanya kazi kwa weledi na kuacha kufika ofisini ‘kuchati’ katika mitandao ya kijamii na kuondoka, badala ya kufanya kazi.

Wakati huo huo, alitoa onyo kwa wanaotumia namba zake za simu kufanya utapeli na kusema atawachukulia hatua za kisheria.
 
Aseme na waliouza nyumba za serikali kiholela wazirudishe ili tuamini kwl yeye ni waziri anayefuatilia mali za serikali maana boss wake ndio alikuwa kinara wa kuuza nyumba hizo
 
ndio maana naona viongozi wa tz ni wanafiki inakuaje unamwambia lipa ukishindwa nakutaja kwenye media, kwa nini wanashindwa kuchukua maamuzi sahihi? na ukiwataja kwenye media ndio utakua umefanya nn?
 
ndio maana naona viongozi wa tz ni wanafiki inakuaje unamwambia lipa ukishindwa nakutaja kwenye media, kwa nini wanashindwa kuchukua maamuzi sahihi? na ukiwataja kwenye media ndio utakua umefanya nn?
Unadhani kutajwa kwenye vyombo vya habari ni mchezo?!?! Aidha nadhani ni utaratibu hivyo baada ya kutajwa hatua stahiki zitafuatwa. Hebu teseme ukweli je wewe ungethubutu kusema la kuwapa mwezi mmoja?!?!? Jamani Serekali hii inathubutu hebu tuiunge mkono wewe unadhani kwa nini madeni hayo moaka leo yapo. Hebu tupe mfano wewe ungefanyaje startight undeenda mahakamani kuwafungulia kesi au?!?!
 
Back
Top Bottom