Mba kichwani (Dandruff): Fahamu Chanzo, tiba na jinsi ya kuepukana nazo

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI:
Wanajamii natumaini hamjambo.

Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya Mba. Nimejaribu kutumia dawa mbali mbali ikiwa ni pamoja na shampoo pamoja na kuosha nywele mara 3 kwa siku lakini bado naona mba haziiishi.

Naomba mnisaidie ni dawa gani nzuri kwa ajili ya Mba.

Asanteni.
---

---
Hivi wadau mba ni nini? Kitu gani husababisha mba za kichwani? Mfano mimi nina nywele fupi na ninajitahidi sana usafi lakini bado mba wananisumbua na kichwa huwa kinaniwasha nikijikuna na kitana unabaki ungaunga unaoashiria ni mba..je nifanye nini?
---

UFAFANUZI WA KINA WA TATIZO LA MBA KICHWANI (DANDRUFF):

Mba ni ugonjwa wa ngozi unaowapata watu wengi na kusababisha kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi kama ukurutu, ambavyo huweza kukudhalilisha, kuwasha na kuuma muda mwingine. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kwa matunzo mazuri ya ngozi na kichwa.

Kisayansi, kawaida ngozi hujimenya seli za ngozi ziliyozeeka, na hizi seli hupotea bila kugundulika. Vipande vidogo vya mba vinasababishwa na ongezeko la seli za ngozi katika kichwa, ongezeko hili husababisha pia ongezeko la seli za ngozi zilizozeeka kutolewa. Seli hizi zikikutana na mafuta kwenye nywele na kichwa, pamoja zinaonekana na kufanya mba. Mba huchangia sana kukatika kwa nywele na kufanya nywele zisiwe na afya nzuri au kukua vzr.

UTAGUNDUAJE KUWA UNA MBA
Kubanduka kwa ngozi ya kichwa kwa kasi(Kubanduka huku kuna ambatana na kuwashwa kwa ngozi ya kichwa, ambapo inapelekea kuwepo kwa vipande vidogo vidogo vyeupe vya ngozi(ukurutu) kwenye kichwa, nywele na mabega.

AINA ZA MBA KICHWANI
Kuna aina mbili za mba katika kichwa:
- Mba wa kawaida/ wastani aina hii inaweza kutibika kwa matumizi ya shampoo, na tiba asili za kutengeneza nyumbani kama vile mafuta ya nazi na juice ya alovera, castor oil, juice ya limao n.k

- Mba mkali au uliokithiri, aina hii ya mba katika kichwa inaambatana na kuwashwa kwa kichwa, kuvimba na uwepo wa mba wenye urefu sawa na nywele za kichwani. Mba katika hatua hii unaweza kutibika kwa dawa zilizoshauriwaa na wataalamu wa afya.

MBA UNASABABISHWA NA NINI?
Hakuna chanzo maalumu kinachojulikana cha mba katika kichwa, ila zipo sababu ambazo zinatajwa na watu kuwa vyanzo vya mba kichwani. Miongoni mwa visababishi vya mba katika kichwa ni kama:
  • Uchafu: usafi duni wa kichwa na nywele ni moja ya sababu za kuwa na mba kichwani, ni vema kusafisha kichwa na nywele mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kwa wiki kama nywele zako ni ndefu
  • Kutumia mafuta ya mgando kichwani ambayo yanapelekea kuganda kichwani na kuleta mba
  • Pia unapokwangua mba ndio unapozidi kutapakaa au kusambaa
Vyanzo vingine vya mba kichwani vinatajwa kuwa:
  • Utumiaji wa vipodozi vya nywele sana kama vile gelly za kulainisha nywele.
  • Kuwa na ngozi kavu sana kichwani (spray mchanganyiko wa maji na mafuta kila inapobidi)
  • Kutumia vitu kama chanuo, brash, kitana pamoja na mtu mwenye mba
  • Utumiaji wa hali ya juu wa “chlorinated swimmimg pools”.
  • Utumiaji wa bidhaa zenye chumvi au maji ya chumvi kwenye nywele

MATIBABU YA MBA KICHWANI
  • Mba unaweza kupotea ghafla bila matibabu au unaweza kuhitaji kutunza kichwa na nywele kwa kutumia shampoo isiyo na viambata sumu. Mara nyingine mba katika kichwa unaweza kuchukua wiki nyingi kutibika. Baadhi ya matibabu ya mba wa kichwani yanaweza kuwa ya tiba asili au tiba ya kisasa.
  • Inashauriwa zaidi kutumia tiba ya asili kutibu mba wa kichwani, mojawapo wa tiba hizo za asili ni kama:
  • Mafuta ya nazi original na juice ya kutengeneza ya alovera. Juisi ya alovera inatumika pamoja na shampoo ya kuosha kichwa na nywele na mafuta ya nazi kwaajili ya kulainisha ngozi na nywele.
  • Juice ya limao, juice ya limao ina citric acid inayoweza kushambulia fangasi zinazosababisha ukurutu wa ngozi ya kichwa na pia inasaidia kupandisha juu ngozi zilizokufa juu na kuweza kuzisafisha kwa urahisi.
NB: Kamua limao na upate juice ambayo itatumika kusugua kichwani kisha suuza na maji,fanya hivi kila ukitaka kuosha nywele.
Castor oil original (paka kila asubuhi kwenye ngozi ya kichwa iliyo safi)

UTAJIKINGA VIPI USIPATE MBA
Ni vema kchukua hatua ili kuzuia mba kichwani ili usifikie hatua ya hatari zaidi, Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoweza kufuatwa ili kupunguza au kutokomeza kabisa mba kichwani:
  • Kula kawaida, mlo wenye afya ulio jumuisha matunda na mbogamboga kwa wingi. Punguza vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi kwa wingi.
  • Safisha kichwa na nywele zako walau mara tatu mpaka nne kwa wiki au mara moja kama nywele zako ni ndefu na suuza kwa maji mengi.
  • Epuka vitu vyenye chemicals nyingi kwenye nywele (Tumia vitu vya asili kwa nywele zako kama mafuta ya kupika nyumbani ya nazi, juice ya aloevera, castor oil au juice ya limao kutibu nywele zako).

USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
---
Ponda ponda majani na mizizi ya ufuta kwa pamoja. Chemsha ndani ya maji halafu chuja

Matumizi:
Suuza nywele kwa maji hayo kila unapomaliza kuoga jioni.

Kitunguu thaumu na siki ya tufaha (apple)
---
---
---
---
---
 
Ni mba gani wanakusumbua vibalango, mashilingi, mapunye au mba hawa tunaopata wakati tunasuka nywele?
 
Ni mba gani wanakusumbua vibalango, mashilingi, mapunye au mba hawa tunaopata wakati tunasuka nywele?

Ni kama vipele vipele hivi halafu vinauma sana. Nimejaribu shampoo mbalimbali lakini haviishi. Vinaptea kwa muda halafu vinarudi tena. Tafadhali naomba msaada wako manake vinakua kama ni mashilingi hivi na hivyo yanafanya nijisikie vibaya sana
 
Mimi nakushauri bora uende uonane na daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi. utapata ufumbuzi wa tatizo lako. Pole sana.
 
Mimi nimetumia mafuta ya kupaka yanaitwa CONFIDENCE, yamenisaidia sana. Umeshajaribu haya?
 
Nenda upatiwe vidonge Grifulvin or Fulconazole umeze mba wataisha. Mafuta ya confidence, virgin hair, sulphur pia yanasaidia.
 
Wana JF naomba kama kuna yeyote anayefahamu matibabu ya mba unaotokea haswa kichwani kwa watoto wadogo. Nini chanzo chake?
 
Dawa ecxactly siijui ila jitahidi kuwaweka safi muda wote kichwa kisikue na nywele ndefu kwa kuanzia
 
Dawa ecxactly siijui ila jitahidi kuwaweka safi muda wote kichwa kisikue na nywele ndefu kwa kuanzia

au awanyoe ubara.kila nywele zikiota.usafi muhimu.tatizo la jamaa wa hivi watoto wao kila kitu anamuachia hg.mia
 
MBA KICHWANI (DANDRUFF)
Ponda ponda majani na mizizi ya ufuta kwa pamoja. Chemsha ndani ya maji halafu chuja

Matumizi:
Suuza nywele kwa maji hayo kila unapomaliza kuoga jioni.

Kitunguu thaumu na siki ya tufaha (apple)
  • kitunguu saumuumu 3 vikubwa
  • siki ya tufaha (apple cedar).700ml
Ponda vizuri vitunguu saumu tia kwenye siki, koroga vizuri tia kwenye chupa ya bilauri (siplastik) weka kwenye mwanga wa jua muda wa wiki 1.

Matumizi:
Utajipaka kichwani huku ukisugua mara1 kila siku kwa muda wiki 1, baadae utatumia kujipaka mafuta ya zeituni (olive oil) kwa muda wa wiki 1.

Ndimu au siki
Juisi ndimu au siki kijiko1cha chakula weka kwenye glasi 1 ya maji ya kawaida.

Matumizi:
Paka kwenye nywele baada ya saa 1 oshanywele fanya hivi wiki mara 1.

Tui la nazi
Baada kuosha nywele zako vizuri, malizia kwa tui la nazi.

Mbegu za ndimu na pilpili manga
Pondaponda kwa pamoja kwa kipimo sawa

Matumizi:
Paka dawa hii kila siku jioni.
 
Ndugu yangu nashukuru sana kuna mabadiliko makubwa. kitunguu thaumu na siki ya tufaa imesaidia sana.
 
Maradhi ya Mba Hutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell.
dawa zilizopo ni :

Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi.

Fenugreek kwa kiswahili inaitwa (Uwatu) lakini imekaa kama rangi yake ni ya brown imekaa kama Vijiwe jiwe vidogodogo kama kuna Hii Uwatu unachukua vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unaziponda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila taabu yoyote.
 
Jaribu kutumia Selsun Blue shampoo ni maalum kwa mba wa kichwani inaweza saidia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…