Mazingira ni kupanda miti tu?

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
5,054
Reaction score
2,873
Tunakaribia kusheherkea siku ya mzingira duniani kuna swali moja najiulizaga kila siku kuona viongozi wanapanda miti siku hiyo. Maana nijuavyo mm mazingira yanahusu pia kumaneji takangumu, kumeneji majitaka na kupunguza na kuzuia hewa sumu angani. ilikuwa kila ikifika siku hii serikali ije mbele ya wananchi kuelezea wamewezaje kutunza mazingira na wanamipango gani ambayo ipo chini ya uwezo katika kutunza mazingira(tusahau kuhusu hela za wahisani hapa). Kwa mm maoni yngu serkali ingejikita kwnye mfumo wa majitaka na utabibu wake haswa sehemu zenye idadi kubwa ya watu(mjini).Na hii ingesaidia sana kuongeza mapato kwnya mamlaka za majitaka na majisafi na pia kupunguza magonjwa yatokanayo na kutotibu majitaka.Maana sehemu kubwa za miji yetu hazina mfumo wa majitaka. Kwnye suala la takangumu serikali ingetoa msisitizo knye utafiti wa takangumu knnye suala la mbolea ya mboji haswa kwnye takangumu zenye organiki na kuwekeza knye recycling ya takangumu.pia iwekeze knye kujenga landfill hii itasaidia knye kuvuna gesi na kuzuia uchafuzi wa maji ya chini ya ardhi ambayo husababishwa na taka hatarishi. Knye hewa za sumu NEMC iwajibike knye kuwafanya wnye viwanda wawe na vifaaa vya kupunguza hewa chafu kama scrubber na vingeneyo na mipango miji iwe wakali kwnye maeneo ya viwanda kusiwepo na makazi ya watu na makazi ya watu pasiwepo na viwanda na kuhusu upanadaji wa miti tuendelee nao kama kawaida.Tukifanikiwa haya tutakuwa tumeifanyia vyema siku ya mazingira duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…