Maximo atangaza vikosi viwili - yanga 1 & 2

Maximo atangaza vikosi viwili - yanga 1 & 2

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Kocha wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo ametangaza vikosi viwili vya timu hiyo huku kipa Juma Kaseja akitupwa kikosi cha pili.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, anaendelea kuiandaa timu yake kwa ajili ya msimu mpya, lakini ameamua kutengeneza vikosi viwili.

Ingawa amekuwa akifanya siri, katika mazoezi ya Yanga, Maximo ameamua kutengeneza vikosi viwili ambavyo vitaifanya Yanga kuwa na uhakika kwa msimu mzima.

"Kocha amefanya uchunguzi wa kila kitu ikiwa ni pamoja na kuangalia wachezaji wa kigeni kupitia mechi tulizocheza."Hadi sasa anajua uchezaji wa Niyonzima, Kiiza na wengine. Okwi anamjua tokea akiwa Simba, hivyo anapanga kwa uhakika na Simba, hivyo habahatishi," kilieleza chanzo cha uhakika.

Maximo amewapa nafasi wachezaji wote walio katika kikosi cha Taifa Stars ambao watacheza katika kikosi cha kwanza kama ifuatavyo.

Kikosi cha kwanza; Deogratius Munishi ‘Dida', Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro', Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Mrisho Ngassa, Haruna Niyonzima, Coutinho, Jaja na Kiiza/Okwi.
Wachezaji hao wa Stars watachanganywa na wale wa kulipwa huku namba 11 akiwa bado hana uhakika kati ya Okwi na Kiiza, nani atabaki.

Kikosi cha pili kitakuwa ni kile cha wachezaji wengi ambao hawako timu ya taifa na anaendelea nao na mazoezi.

Lengo la Maximo ni kuongeza ushindani na baada ya muda atakuwa akiangalia ni yupi anafanya vizuri anampandisha kwenye kile kikosi cha kwanza, anayevurunda anashushwa kikosi cha pili.

Kikosi cha pili; Juma Kaseja, Saleh Abdallah, Patrick Ngonyani, Rajab Zahir, Juma Said ‘Makapu', Omega Seme, Salum Telela, Hussein Dilunga, Jerry Tegete, Said Bahanuzi na Hussein Javu.

Wanaobaki benchi ni Mustapha Ally ‘Barthez' na mkongwe Nizar Khalfan ambaye alipata nafasi kubwa ya kufanya vizuri wakati Maximo akiwa kocha wa timu ya taifa.

Hata hivyo, Maximo ameamua atakuwa akichanganya vikosi hivyo kuunda kimoja katika baadhi ya mechi kutokana na mambo mawili.

Kwanza kuwapa nafasi wachezaji hao kucheza pamoja, lakini kuwapa nafasi vijana nao wacheze ili kuwakuza, ambayo imekuwa ni sera yake.

Chanzo: Global Publishers
 
anajua kazi yake iliyobaki ni wachezaji kujituma uwanjani tu.
 
...wachezaji wa kikosi na mbili inabidi wajitume sana, ili wapate nafasi ya kucheza kwenye kikosi #1
 
Watu wa habari wawache kuwaibia wasomaji kwa kuwauzia habari viza (junk). Na wasomaji nao wasjitoe kirahisi kwa matapeli hao kwa kuvutiwa tu na mtu, timu, kitu au jambo wanalolipenda wakiliona kwenye kichwa cha habari. Hivi sasa Simba, Yanga, Maximo, Coutinho, Lugarusic, Jaja, ndi mpango mzima wa vichwa vya habari kutapeli wanunuzi wa magazeti. Mengine in UKAWA, CHADEMA, CCM, Bunge la Katiba, mabomu. Kwa wagonjwa wa timu za ughaibuni wao wakishaona tu majina ya timu ama wachezaji wanaoshabikia kwenye kichwa cha habari, tayari wameshanunua. Nadhani wakati umefika kwa Baraza la Habari kuwaruhusu wanunuzi magazeti kurejeshewa fedha zao pale vichwa vya habari vinapotofautiana kwa asilimia kuanzia 50 na habari zilizo chini yake. Labda wizi huu wa kiinimacho utatupungukia, na uwajibikaji kwa wahariri utaongezeka.
 
Back
Top Bottom