Smith Kiombo
Member
- Jun 15, 2023
- 28
- 45
Kama una usimamizi mzuri uza vinywaji vya jumla.
Pombe kali, bia, soda, juice nk.
Kama ukiwiwa basi pia hilo duka lako liwe na mahitaji ya nyumbani jumla na rejareja.
Kua na vijana wa usambazaji kuanzia wawili, ila kwa kuanza anza na mmoja unaemfahamu vyema na kumuamini then utaongeza wengine kadri ya mahitaji.
Fungua hiyo biashara eneo ambalo ndio linakua na halina upinzani mkali ili uvune wateja wengi.
Wateja wa biashara hii wengi ni wa kudumu, inakua kama wanakufanyia biashara kama utakua vizuri kuimaintain.
Kazi kwako.
Mnapelekaga wapi akili
Nakushauri Fanya biashara ya restaurant,
Uza vyakula vikavu ,,,,
Kama
Chips
Burger
Kuku crunch,
Bites
Fresh Juice Tu!
Vitu vya kuzngatia ni kama
Eneo lenye watu wengi na parking iwepo baasi. Ubunifu mzuri wa kisasa wa ofisi.
Mtaji ni 150M???
Toa ajira watu wakuuzie business idea zao.
Ila biashara zote zinazokuwa ulimwenguni zinatoka moyoni sio kwenye mashauri
Rubiii Mwaa😘Mtaji ni 150M???
Toa ajira watu wakuuzie business idea zao.
Ila biashara zote zinazokuwa ulimwenguni zinatoka moyoni sio kwenye mashauri
nimeipenda hii... naiibabiashara zote zinazokuwa ulimwenguni zinatoka moyoni sio kwenye mashauri
Sio shida sehemu kama Dodoma ambapo watu ndo wanawekeza sana na mji ndio unakua, ni issue ya research Tu mkuu.kupata location inayochangamka siyo shida?
Fungua phamarcy i lkubwa na ya kisasa eneo lililochangamka utakuja nishukuru baadaye
nimeipenda hii... naiiba
Wazo sina endelea kusubiri yanakujatoa wazo tu dada yangu ikiwa nzuri tufanye kazi, kama wazo lako ni private basi niandikie inbox
Mwaa😘Mwaa😘Rubiii Mwaa😘
Yapuna uzoefu na hii biashara?
Kuna mashamba ya mpunga mkoani Mbeya wilaya ya Mbarali yanakodishwa kwa Kilimo cha mpunga waweza fanya uwekezaji na ukazalisha.Habari zenu wana JF, Naamini wote ni wazima wa afya.
Mi ni kijana mpambanaji na kwenye harakati za utafutaji nikajikuta niko nje nchi na ni mda sasa tangu nilipotoka tz, Mungu amesaidia nimekusanya 150M ambazo napenda kuwekeza lkn kwa sababu nimekaa nje kwa mda mrefu sasa na mambo mengi yamebadilika.
Nilikuwa naomba ndugu zangu ni biashara ipi ambayo naweza nikaanza na huo mtaji na ikanitoa( 150M) naamini kuna watu wana mawazo mengi na mazuri lkn hawaja jaliwa kuwa na mitaji na kuna wengine wameanza lakini si kwa ukubwa wanao utaka kutokana na mitaji yao. karibuni kwa mawazo
Nb: kwa atakaye leta wazo nzuri na nikalipitisha tutafanya kazi pamoja au kulinunuwa kabisa wazo lake. Asanteni na karibu kwa mawazo