Mawazo na ushauri wenu wana JF

Syston

JF-Expert Member
Nov 6, 2017
243
339
Habarini, natumai mu wazima, nimekuja kwenu nina jambo langu nahitaji ushirikiano wenu.
Kwa kuanza mie ni designer nadili na Mechanical & Electronics. upande wa mechanical nadesign anything unataka using SOLIDWORKS, INVENTOR & NX, pia sijaitupa mkono AutoCAD maana ndo ilonikuza. Ukija electronics na deal sana na embedded systems na mainly napendelea PIC microcontroilers & ARM Cortex M series.

Kutokana na experience yangu nimeona kuna uhitaji mkubwa wa elimu katika hizi embedded systems na watu wengi wanajifunza kwa ARDUINO development boards. Sio wote wanaweza kumudu gharama za arduino japo hapa bongo zinapatikana kwa bei affordacle ila mie nikaona si vibaya kama tukaishusha zaidi hiyo bei, kwa mfano mtu akaweza kujipatia board kwa angalau kwa 2/3 ya bei ya sasa. Lakini pia kuhakikisha elimu hii haipatikani vyuoni pekee ili tuweze kuwa na wataalamu wa kutegemewa baadae.

Wengi hapa ni mashahidi, tumeshuhudia wabunifu mbalimbali wakitangazwa kubuni vitu lakini mwisho wa siku wanapotea, mfano kuna mdada nimemsikia weekend ilopita amebuni SMART DUSTBIN, ni idea nzuri lakini wapo wengine kama huyu wanashindwa kuingia sokoni kwa sababu upatikanaji wa vifaa una gharama kubwa kuzidi makadirio ya soko la bidhaa hasa katika hii sekta ya teknolojia katika electronics, fikiria bidhaa yako unatakiwa uiuze 20000 ila inabidi utumie 30000 kuizalisha, huwezi enda popote.

NINI SULUHISHO
Ili kukabiliana na hali kama hii inabidi kuwe na local manufacturing ya hizi bidhaa ambazo wabunifu wetu wanazitumia sana katika kubuni solutions kutatua changamoto katika jamii.
Kama nilivyotangulia kusema mie ni designer na tayari nimeshalifanyia kazi hili isipokuwa nimekwama katika na ninahitaji ushirikiano na ushauri katika mambo yafuatayo;

1. Natafuta team ya watu 4 walio tayari tufanye hii kazi, kati yao lazima awepo website designer (kuna website niliyo design atatakiwa kuipitia na kuiweka sawa), awepo mtu anaejua electronics viruzi atakuwa ana design circuit na PCB from scratch. Kama unaweza ku create bootloader i would like a hand na utakuwa na priority.

2. Biashara hii inahitaji mtaji wa kuanzia angalau milioni 10 ila kama unavyojua wenye akili hawapewi pesa hivyo unahitajika ufadhili aidha kwa mfumo wa uwekezaji au mkopo, kwa hivyo kama team tutashirikiana kutafuta njia za kupata mtaji huo.

3. Ninaomba kuwaalika wana JF katika harambee ili kufanikisha jambo hili tuwasaidie vijana wetu na tutengeneze nafasi za ajira maana biashara kama hii huko kwa wazungu zinaajiri kuanzia watu 35 na kuendelea.

Harambee itafanyika pale tu team itakapokuwa timepatikana tayari na itatambulishwa hadharani humu JF.
 
Back
Top Bottom