Mawaziri wa Kikwete wanasema uongo

Mawaziri wa Kikwete wanasema uongo

DUNIANGUMU JR

Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
43
Reaction score
14
MAWAZIRI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUSEMA UONGO NI SERA YA SERIKALI AU NI SERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI? JE WATANZANIA NI YEPI WATAJUWA NI YA UKWELI AU UONGO?

Hali hiyo ilitokea juzi wakati Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo (Tatoa), walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu pamoja na mawaziri kuzungumuzia pamoja na mambo mengine ni kero za watumisha wa wizara hiyo kwa kuwasumbuwa wafanyabishara hao kwa kuomba rushwa kwa kila kitu inafikia mahali hata faida ya biasha hiyo inakuwa hakuna tena.

Kuhusu kero ya matuta, Naibu waziri Gerson Lwenge alielezea kuhusiana na kero ya matuta yaliyowekwa katika barabara, alisema tayari wameshaanza kuondoa matuta kwenye barabara nyingi nchini ambayo yamekuwa ni kero kwa wasafirishaji.

Hata hivyo, alikumbana na swali la mpopoo kutoka kwa Mbunge wa kigoma mjini ndugu Peter Serukamba likimtaka atoe
mfano wa barabara ambazo matuta yameondolewa na ndipo alipotaja barabara ya Dar es Salaam kwenda Dodoma. Baada ya majibu hayo Mbunge huyo wa Kigoma alimtolea uvivu bila kujali wote wanatoka chama tawala na kusema “Mimi Mheshimiwa waziri Lwenge nimepita hapo juzi kuja hapa Dodoma, matuta yapo vile vile,” alisema Serukamba, hali iliyomfanya waziri kubadilisha kauli yake kwa kukiri kuwa hayajaondolewa.

Mkazi mmoja wa mji mwema mjini Dodoma Ndugu Mugaya Kalolo alishangaa kuona watendaji wa serikali wenye dhamana wanasema uongo kiasi hicho mbele ya watanzania bila uoga wowote, "sasa fikiria kama waziri anawambia wananchi wa kijijini ambao hajasafiri kupita njia hiyo ni lazima wataamini alichosema waziri" kwa mfano huo huo waziri wa serikali anaweza kusema wizara yake inahitaji mabillioni ya pesa kwa ajili ya shughuli za maendeleo kumbe ni uongo ni maendeleo yake na familia yake, aliendelea na kusema, Hii tabia ya kusema uongo kwa mawaziri wa serikali inasabishwa na kutowajibishwa kwa hiyo wanaona nikama fashion.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom