Mawaziri wa awamu ya tano mnamtakia mema rais Magufuli??

K M S

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
524
424
Binafsi napata tabu kuwaelewa watendaji wa serikali haswa mawaziri. Mmekuwa watu msio wakweli sijui hamjiamini au ni vipi. Mmekuwa hamtoi taarifa za kweli kwa umma katika mambo ya msingi haswa zile changamoto zinazowakabili wananchi.

Hapo nyuma kulikua na tatizo la chanjo mahospitalini magazeti yakaandika, mawaziri husika wakakanusha baadae ikabainika ni kweli mkaanza kukimbizana kupeleka hela. Baadaye tukaskia kipindupindu, mwanzo mkakanusha baadae waziri akaja na maelezo kuwa ma RC wanaficha taarifa kuogopa kutumbuliwa.

Haya hili la njaa mmekanusha wee sasa sauti zimeanza kuwa kubwa sasa tuwaeleweje au mnataka kumhujumu bosi wenu manake inaonekana hamumwambii ukweli wa hali halisi iliopo nchini katika mambo mengi.
 
Wamemfahamu kuwa ni mtu anayependa kuelezwa Yale anayopenda kuyasikia, kwa hiyo ndicho wanachokifanya
 
Ukweli ninachokiona mimi Mawaziri ,Wakuu wa mikoa,Wakurugenzi,Wakuu wa wilaya wanachokifanya ni kumfurahisha aliyewateua badala ya kuondoa kero zinazowazunguka wananchi.Utashangaa jambo la kiutendaji ndani ya ofisi wanaitwa waandishi wa habari ili mtu aonekane anachapakazi.
Badilikeni wateule ili wananchi wafurahie utendaji wenu wa kazi.Sasa hivi njaa/ukame upo kila mkoa lakini huoni kiongozi akitoka kuwapa ushauri wananchi wafanye nini wao kila kukicha ni matamko tu bila ya utafiti.
 
Binafsi napata tabu kuwaelewa watendaji wa serikali haswa mawaziri. Mmekuwa watu msio wakweli sijui hamjiamini au ni vipi. Mmekuwa hamtoi taarifa za kweli kwa umma katika mambo ya msingi haswa zile changamoto zinazowakabili wananchi.

Hapo nyuma kulikua na tatizo la chanjo mahospitalini magazeti yakaandika, mawaziri husika wakakanusha baadae ikabainika ni kweli mkaanza kukimbizana kupeleka hela. Baadaye tukaskia kipindupindu, mwanzo mkakanusha baadae waziri akaja na maelezo kuwa ma RC wanaficha taarifa kuogopa kutumbuliwa.

Haya hili la njaa mmekanusha wee sasa sauti zimeanza kuwa kubwa sasa tuwaeleweje au mnataka kumhujumu bosi wenu manake inaonekana hamumwambii ukweli wa hali halisi iliopo nchini katika mambo mengi.
mkuu pia hawajui wafanyalo km huyu.Halafu yupo ktk siasa zilizomzidi uwezo wa kiakili na kiustaarabu. Kuhusu Ghala la Chakula: Huyu mkuu wa mkoa Arusha atuweke sawa
 
Ukweli ninachokiona mimi Mawaziri ,Wakuu wa mikoa,Wakurugenzi,Wakuu wa wilaya wanachokifanya ni kumfurahisha aliyewateua badala ya kuondoa kero zinazowazunguka wananchi.Utashangaa jambo la kiutendaji ndani ya ofisi wanaitwa waandishi wa habari ili mtu aonekane anachapakazi.
Badilikeni wateule ili wananchi wafurahie utendaji wenu wa kazi.Sasa hivi njaa/ukame upo kila mkoa lakini huoni kiongozi akitoka kuwapa ushauri wananchi wafanye nini wao kila kukicha ni matamko tu bila ya utafiti.
Kwa utaratibu huu nchi itakwenda kweli? Atakuja kushtuka limeshazama
 
Back
Top Bottom