Mavugo na Chirwa wawe fundisho kwetu watanzania

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Wachezaji Obrey Chirwa anayechezea timu ya Yanga pamoja na Mavugo wa simba wanatakiwa wawe fundisho kwa wapenzi na mashabiki wa soka Tanzania.

Watanzania tunapenda sana njia ya mkato, tunapenda matokeo mazuri yaje kwa haraka bila subira wala kuvuja jasho. Ujio wa mavugo na chirwa katika vilabu vyetu vya soka hapa Tanzania viliambatana na kiwango kidogo kwa wachezaji hao hii kutokana na mabadiliko ya mazingira kwa wachezaji hao pamoja na mabadiliko ya ligi yenyewe.

Wachezaji kutokuweza kwenda sambamba na mabadiliko ya mazingira na ligi kwa ujumla si la Tanzania tu, mchezaji tegemeo leo wa Mancheater united Hennry Makhtryaian anayecheza namba kumi alikuwa tegemeo katika timu ya Dortmond ya huko ujeruman lakini alianza vibaya ligi la uingereza na kufanya asipangwe kabisa kucheza chini ya kocha Jose Mourinho lakini mashabiki wa man united walikuwa pamoja naye na waliamini atazoea mazingira na ligi hiyo, Leo hii ni mchezaji Tegemeo wa timu ya machester united.

Sasa kwa watanzania hatuna uvumilivu kwenye soka Mavugo hakuanza vyema kuitumikia timu ya simba kitu kilichopelekea asiwe anacheza mara kwa mara lakini mashabiki wa simba kupitia mitandao ya kijamii tulikuwa tukiporomosha matusi, kebehi, Dharau na majungu Sana juu yake na matokeo yake leo tunajisikia aibu hata kumsifia, hali kadhalika mchezaji Obrey Chirwa wa timu ya Yanga .

Rai yangu kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya mpira hapa Tanzania tuchukue mafanikio haya kama fundisho, mpira si hesabu kwamba leo ukijua 800 + 800 = 1600 nchi zote dunian ukienda utapata jibu hilo. Mpira ni sanaa inabadilika badilika kulingana na mazingira na jamii ya sehemu husika. Mungu Ibariki Tanzania
 
Tatizo huwa ni sifa wanazomwagiwa wakati wa usajili na dau kubwa wanalopewa wakifika uwanjana hawaoneshi tofauti na wazawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom