Mavazi ya bikini yasababisha maonyesho kupigwa marufuku Guinea

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Serikali Guinea imepiga marufuku kwa muda maonyesho ya urembo baada ya mavazi ya bikini kuzua shutuma nchini humo.

Wagombea walijipanga mbele ya waziri mkuu Mamady Youla wakiwa wamevaa bikini siku ya Jumamosa na kasababisha shutuma kwenye mitandao ya kijamii.

Gazeti moja liliandika likiuliza ikiwa waziri mkuu alikuwa akiunga mkono ukahaba.

_94648459_beautypeagent.png

Waziri wa tamaduni anasema kuwa marufuku hiyo itasalia hadi pale vipengee vipya vya maadili vitatangazwa.

Amasema kuwa kamati imebuniwa kuandika viprngee hivyo.

Pia amesema kuwa serikali imefuta mikataba na waandalizi wa maonyesho hayo ya urembo.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Wawafungie tu....sio utamaduni wetu waAfrica kuonyeshana nguo za ndani,huwa nashangaa sana baba upo nyumbani unaangalia Tv mara unamuona mwanao anapita na kichupi jukwaani.mie hiyo chupi ya dada'angu kwenye kamba siitoi hata kama mvua inataka kunyesha then leo nikaone akiivaa anafananaje.!hapana aisee.
 
Tatizo letu waafrika ni moja ju. Hatuna kitu chochote ambacho kiko documented kinachoitwa maadili/utamaduni..
Ni fikra tu za watu ambao hat ukiwauliza hicho wanchoita maadili ni nini hata hawajui sana sana utakuta ni imani za kidini na kila mmja ana imani yake

Qoute:
Waziri wa tamaduni anasema kuwa marufuku hiyo itasalia hadi pale vipengee vipya vya maadili vitatangazwa.

Amasema kuwa kamati imebuniwa kuandika viprngee hivyo.

Pia amesema kuwa serikali imefuta mikataba na waandalizi wa maonyesho hayo ya urembo.

Chanzo: BBC/Swahili

Hivyo vipengele vipya anavyovitunga waziri wa utamaduni atakuwa amekaa na nani kujadili?
Je wananchi watapewa nafasi ya kuafiki hicho walichoandaaa au ni matamko tu!!!!!

Viongozi wetu wanatakiwa watambue kuwa kiongozi ni kuonyesha njia..na kuanda mazingira ambayo wananchi watashiriki...
 
Mkuu jubilant unataka kutuambia kwamba pamoja na kiswahili sahihi ulichoandika hapa hata wewe hujui ninini hasa maana ya maadili?kama unae mwanao wa kike unadhani ni sahihi kwenda kuvaa kichupi na kupita nacho hadhrani mbele ya wanaume wenzako na kaka/wadogo zake wakimtazama?sometimes hata wewe mwenyewe baba kwa bahati mbaya unaweza kumuona{siijui jinsia yako nimetumia zaidi wanaume maana ndo mara nyingi tunaojali mavazi wanawake hawajui ninini hasa cha kuvaa ikiwa wengine wanatembea mitaani uchi}
 
Mtazamo wangu ni sawa kabisa na wewe kwa imani yangu siwezi kuruhusu hilo litokee.
Ninachotatizika mimi ni kwamba hatuna any system in place ambayo inatuongoza na ndio maana utaona mpaka maandalizi hayo yamefanyika ni kwamba hakuna system yoyote inagoguide..
Inatakiwa katiba ya nchi ndio itoe muongozo wote huo. hilo ndio tatizo tu langu why we acts after?? matamko??

Kuvaa hizo bikini inpublic kwangu napata wakati mgumu sana kuamini ninachokiona na wala sifurahishwi nacho, sio kwa mwanangu ni kwa mtu yeyote yule. ni mtizamo wangu tu wa kiimani na kwa tamaduni nilizolelewa nazo enzi za nyerere...
Lakini enzi hizi ndugu!! taabu kweli kweli mambo ya ingia istagram unabaki ukijiuliza ndio wapi tena huko?
 
Wawafungie tu....sio utamaduni wetu waAfrica kuonyeshana nguo za ndani,huwa nashangaa sana baba upo nyumbani unaangalia Tv mara unamuona mwanao anapita na kichupi jukwaani.mie hiyo chupi ya dada'angu kwenye kamba siitoi hata kama mvua inataka kunyesha then leo nikaone akiivaa anafananaje.!hapana aisee.
Unaijua asili ya nguo za mababu zetu wewe kweli?!!
 
Wawafungie tu....sio utamaduni wetu waAfrica kuonyeshana nguo za ndani,huwa nashangaa sana baba upo nyumbani unaangalia Tv mara unamuona mwanao anapita na kichupi jukwaani.mie hiyo chupi ya dada'angu kwenye kamba siitoi hata kama mvua inataka kunyesha then leo nikaone akiivaa anafananaje.!hapana aisee.

eti sio utamaduni kuonesha nguo za ndani wakati waafrica walikua hawavai hata nguo bila mzungu hata izo chupi tusingekuwa nazo, utamaduni wa mwafrika ilikuwa kuvaa magogo na ngozi kuziba sehemu za chini sehemu zingine zote zinakua wazi
 
Back
Top Bottom