Katika maisha kuna kujitambua, kujua unachoweza kufanya na kukifanya kwa bidii. Ukifanya hivyo utafanikiwa na kuweza kusimama wewe kama wewe na muhimu zaidi kitakupa ujasiri na furaha ya kutoka moyoni. Utaweza kuwasaidia ndugu zako na kupata heshima toka kwa jamii na kuwa na mahusiano thabiti. Hakuna mwanaume atakayechezea hisia zako akijua wewe ni mtu wa maamuzi na jasiri.
Pia unapoingia katika mahusiano jua unachokitaka na simamia haki yako. Pia jua akikufanya ulie ni kosa lako na ni wajibu wako kutovumilia mazingira hayo ya kulizwa. Ni wajibu wako kusimamia faida ya nyote wawili kwenye uhusiano, usimuonee na asikuonee. Kwa sababu kama kuishi wawili kunakuumiza kuliko kuishi mwenyewe, what is the point of the relationship?
It is your life, it is your decision