maumivu makali yanatesa moyo wangu


mkuu ufaham wako ukojuu. maneno yako yageuke kuwa MAOMBI iwe NEEMA Kwangju.Hekima ya MUNGU iwenawewe daima.
 
pole mkuu katika kipindi kigumu ulicho nacho. Hakuna njia mbadala zaidi ya kumtegemea Mungu na sali sana ili upate faraja ya kweli,Mungu wetu ni mwema soon hy hali itapotea maana wewe ukiwa hivyo na watoto watakuwa kwenye hali gani?

Nimekubali ushauli wako kiongozi .ukwelinikwamba nilikuwambali sana nikawa najiuliza kwanini watu wanakufa.?
 

Punguza speed unapokuwa unaandika ili uandike maelezo yanayoeleweka

Kuhusiana na nilichokushauri tanbua kuwa nimekushauri kile ninachoona mimi ni sahihi na unaweza kuacha kama unakiona hakifai

Lakini nakuambia kuwa wewe hujitendei haki na hata huyo mpendwa wako aliyetangulia mbele ya haki humtendei haki pia

Unaweza kuwa unatamani upewe ushauri uliokuwa unautarajia wewe lakini huo sio ushauri unaostahiki

Chukulia mfano mgonjwa wa malaria huwa ana kawaida ya kupenda kuota jua kali na hicho ndicho anachokifurahia,je yupo sahihi?

Wewe hapo utawaona wale watakaokuonesha huzuni kwa kuwa kiukweli una njaa ya huruma ilimujisikie vyema lakini huko kujisikia vyema ni kwa muda tu na hali itarudia

Jifunze kukubaliana na mambo na kukubali yaende!
 
Mtoa mada pole sana lakini ushapata wa kukufariji huyu amejitokeza naimani utasuuzika nafsi

sasa hajapatikana. nilichokiona kwaumri sawa na wangu. namaanisha lika kuanzia miaka 30.hasa wazuri WALiSHAUMIZWA Hawaamini kabisa kama anaweza kupendwa. na kupeda hiyo ndo changamoto.
 
Inasikitisha sana mtu wa umri kama huu kuondokewa na mpendwa wake miezi mitano iliyopita halafu analialia kiasi hiki

Ndugu, mioyo ya binadamu inatofautana, uwezo wa kukabiliana na matatizo haufanani...
Tujaribu kumpa njia m'badala ya kukabiliana na majonzi alonayo.
 
Ndugu, mioyo ya binadamu inatofautana, uwezo wa kukabiliana na matatizo haufanani...
Tujaribu kumpa njia m'badala ya kukabiliana na majonzi alonayo.

Hakuna njia mbadala tofauti na kumweleza ukweli!
 
Pole zako Mkuu inaelekea ulikuwa unampenda sana Mkeo, lakini yaliyotokea ndio yameshatokea na kama ulivyosema maisha ni lazima yaendelee. Ni kawaida kuumia kiasi hicho inapotokea mahusiano na yule uliyempenda kuvunjika. Kila la heri katika kuendelea na maisha yako.
 
Pole sana kwa kuondokewa na ubavu wako Jambo Moja binadamu tunashindwa kulikubali kwamba hakuna kitakachobaki hapa duniani yeye katangulia tu na wewe utafuata cha umuhimu ni kumshukuru Mungu na kukubali kwamba vyote vyake, jiombee wewe sasa kwani mwenzio safari yake imeisha kazi kwako jipange na iko siku utakuja hapa utasema nimempata mwingine na kuomba ushauri hapa jaribu. usifananishe yule ni yule tu.kubali matokeo na uombe upate mwingine si kama bora zaidi ya yeye hayo ndio maombi zingatia.kila la kheri
 
Pole sana aisee.Mie naelelewa nini unamaanisha.Nimempoteza mme wangu kipenzi Mwezi wa Nane mwaka huu.Kweli asikwambie mtu.adi leo sijazoea kabisa.Pole sana mwenzangu.
kaniachia mtoto mmoja na umri wangu ni 32.Nipo kwenye wakati mgumu sana aisee.adi nimepata ugonjwa wa moyo. khaaaa kweli kifo cha umpendae ni matatizo makubwa. Pole sana mwenzangu.

karibu tushauriane na kupeana mawazo ya hapa na pel hasa kwenye mambo ya mirathi na nk maana ndo yanayotukabili wengi.
 
Pole ndugu,kuondokea na kipenzi cha moyo wako ni maumivu makali sana. Lakini yakupasa kujipa moyo na maisha yaendlee kama ulivosema,kama walivoshauri wengine penda kujichanganya na wengine,uwe mtu wa ibada taratibu mzigo wa maumivu yatapungua. Na Mungu atakupa mke mwingine atakaesuuza mtima wako. Muhimu ni kua makini usijeangukia kwenye janga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…