Maumivu chini ya ziwa upande wa kushoto

reina

Member
Aug 11, 2011
52
8
Hello experts, naombeni mchango wenu juu ya hili. Mara nyingi nikiwa na mawazo sana ama kuumizwa na jambo sana huwa napata maumivu makali chini ya ziwa upande wa kushoto.maumivu huwa kama kitu chenye ncha kali na huzidi pale ninapovuta hewa ndani.mara nyingine maumivu husamba mpaka kwenye mkono wa kushoto na mgongoni.kuna kipindi sikuweza kabisa kulalia upande wa kushoto kwani maumivu yalikua yanazidi. Ila nikiwa na furaha na amani bila mawazo hali hii huisha.je ni kitu gani hiki?
 
Mimi nilikuwa natatizo kama hilo nilipoenda hosp nikaambiwa ni dalili za vidonda vya tumbo,Nikapewa dawa zinaitwa fontacid,niko poooa!nenda hosp utapimwa utapewa dawa sahihi!
 
mara nyingi huwa ni dalili za vidonda vya tumbo au blood pressure wahi hhospital upate matibabu
 
Hello experts, naombeni mchango wenu juu ya hili. Mara nyingi nikiwa na mawazo sana ama kuumizwa na jambo sana huwa napata maumivu makali chini ya ziwa upande wa kushoto.maumivu huwa kama kitu chenye ncha kali na huzidi pale ninapovuta hewa ndani.mara nyingine maumivu husamba mpaka kwenye mkono wa kushoto na mgongoni.kuna kipindi sikuweza kabisa kulalia upande wa kushoto kwani maumivu yalikua yanazidi. Ila nikiwa na furaha na amani bila mawazo hali hii huisha.je ni kitu gani hiki?
pole mkuu! dalili un azosema hizo ni za magonjwa ya moyo yaitwayo angina pectoris. hii husababishwa na kusinyaa kwa mishipa ya moyo (coronary arteries), au kuwa na pressure nyingi. kuwa na mawazo mengi ni mojawapo ya sababu zifanyazo kuhamsha kwa ugonjwa huo. inakubidi uende hospital, au uwe dawa iitwayo nitroglycerine, ni vidonge, unaweka kimoja chini ya ulimi napopata maumivu hayo.
swali unavuta sigara? je, ukifanya kazi ngumu maumivu hayo pia huja? pressure yako ni ipi? kuna yeyote katika ndugu zako ana magonjwa ya moyo au amnekufa ghafla? ukikimbia inakuwaje?
 
Back
Top Bottom