kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 17,333
- 21,425
Kwanza nikupe pole IGP na nijipe pole kama raia kwa kupoteza walinzi wetu wa usalama wa raia,bila ya wao kusimamia usalama wetu saa hizi hali ingekuwa mbaya zaidi,
Dhumuni langu ni kuwa jeshi la polisi halifanyi kazi zake katika kiwango cha juu ila ni zimamoto polisi wetu hutumika vibaya tu pindi panapotokea matatizo ya vyama vya siasa na kukabili mtu mmoja mmoja kwa maslahi ya mtu aliewatuma
Sitaki kusema tukio hili ni la kisiasa sababu tusigeuze siasa ni dampo la kutupia kila baya
Jeshi la polisi tanzania hufanya shughuli zake kwa matukio ya muda mfupi mfano wiki hii pametokea ujambazi mwananyamala basi polis watakurupuka na kuvamia mwananyala na kubeba watu wa kata nzima na mwisho wa siku watatafuta chaka huko mbezi watulitee maigizo kuwa wamekamata silaha za kivita pesa,mapanga,pinde na mishale eti kuwa hilo ni chimbo la majambazi
Baada ya hapo wale watu wa mwananyamala wataachwa wakiozea magerezani bila kutendewa haki na waliokamatwa si wahusika na kesi wamebambikiwa bado hiyo haijakuwa na uhasama kwa polisi na jamaa za wale mliowapoteza magerezani kwa kuwaonea
kwanini msimkate mtu mkamuhoji mkihisi hausiki mumuachie lakini wakati huo ukimfuatlia kwa ukaribu lakini polisi wakishatia kijiji ndani wao ndio wameshamaliza hakuna ufuatiliaji
sasa kwa hili linalojiri sasa ni matokeo ya uvivu wa kutofuatilia mambo kwa muda mrefu eneo hilo mlikamata silaha na pesa mkasema ndio waliovamia kituo cha stakishari baada ya hapo ameuwawa mkuu wa polisi akafuata kiongozi wa ccm sasa ni polisi na ndani ya hapo mmeshakamata watu wengi sana bila ya kuwa na uhakika
Na tunajua jeshi la polis linapohoji watuhumiwa hutumia nguvu je bado hamjatengeneza uhasama na raia na ndio wameshaanza hivyo moja jumlisha mbili ni tatu bila kufanya kazi kwa uweledi mambo hayo hayatakoma na yatasambaa nchi nzima
Polisi angalieni utendaji wenu sio kuonea watu na kuwambikia kesi!
IGP waongezeeni askari silaha ikiwa wapo kumi kuwe na silaha kumi sio watu kwenye difenda moja wapo patrol askari kumi bundiki mbili huo ni udhaifu mwingine tujikinge kabla ya hatari!
Aksanteni