Drjacka92
JF-Expert Member
- Jul 20, 2016
- 445
- 522
Wasalaaam!!.
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.
Niwape pole Ndugu wa marehemu askari waliouawa barabara ya Kusini(Lindi, Mtwara).
Kiukweli kabisa tukio la kuuawa askari limeniumiza sana, yani askari nanee!!! inauma.
Matukio haya yanatia hofu sana, si tu kwa wakazi wa maeneo yalipotokea mauaji ya Askari Bali hata wananchi wa mikoa ya kusini Lindi, Mtwara na hata Ruvuma na Songea maana sikuhizi magari ya Songea baadhi yanatumia barabara hii ya Lindi.
Wengi wanaijua mikoa ya kusini kutokana na ubovu wa barabara uliosababisha watu kusafiri sio chini ya wiki moja kutoka Lindi kwenda Dar es salaam tofauti na sasa watu wanaweza kusafiri kwa masaa manne tuu, na hii ni kutokana na Ujenzi wa barabara hasa daraja la Mkapa.
Lakini kwa mauaji haya ya Askari naona kabisa mikoa ya kusini inaweza kurudia ukoloni wakutokuwa na Mabasi yakuwafikisha mikoani kwao.
Leo hawa wauaji wameweza kuwatageti askari nakuwaua, naamini kesho wanaweza kusubiri gari ya abiria nakuipiga tairi ikapinduka ili watekeleze uhalifu wao kitu ambacho kitapoteza uaminifu wa usalama wa barabara hii ya kusini.
Imagine wewe ndiye mmiliki wa mabasi ya kusini, Lindi, Mtwara, Songea na Ruvuma alafu unasikia uhalifu unaendele kutokea katika hii barabara, je, utaendelea kuruhusu basi lako lifanye Ruti ya hii barabara?
Ninachoamini ni kwamba Ipo siku hawa watu (wauaji) watateka mabasi ya abiria nakusababisha madhara makubwa sana, tena bora wasimamishe basi kisha wakusanye pesa kuliko wakapiga risasi tairi mana itatokea ajali kubwa na mbaya mno.
Kitakachotokea huko mbele nikwamba wamiliki wa mabasi watasitisha mabasi yao kufanya safari za hii mikoa ya kusini kwakuwa barabara yao sio salama, kuna wauaji na watekaji.
Jeshi la polisi lifanye jitihada maeneo Yale ya Jaribu mpakani kuwe na Kituo kikubwa cha Polisi Ili tufukuze wale washenzi wa maeneo Yale,.
Pia nimepata dokezo kuwa wakazi wa rufiji hawafurahii lile daraja la Mkapa kwakuwa zamani walikuwa wanafanya biashara sana wasafiri wanapolala maeneo Yale wakisubiri kuvuka tofauti na sasa ambapo mabasi yanapita tu kwaurahisi.
Mikoa ya kusini Ipo hatarini kupoteza mabasi yanayofanya ruti za mikoa hiyo, ni bora ufanye Ruti ya Moro, Dar unakuwa salama kuliko ruti ya Hii barabara.
Askari polisi muwe makini sana, haijalishi unatoka ulinzi au unaingia, kuwa Attention, upo vitani muda wote