Matuta ni physical measure, ni interpretation that watu hawana uwezo wa kufuata sheria bila ya shuruti. Hiyo ndiyo tafsiri ya kila mtu anapokuja Tanzania. Ni aibu kwa nchi, ni aibu kwa wananchi wake.
Matuta ya Bara bara ya Shinyanga - Mwanza ndio funga kazi. Usiombe uwe umepanda basi alafu umekaa siti ya nyuma. Utafika kiuno chote kikiwa kimetenguka. Matuta ya bara bara ya Singida - Dodoma, ndio matuta bora kuliko yote nchi hii. Yani tuta unaweza ukalipanda na spidi sitini bila kurushwa sana. Yana umbo zuri na ni rafiki kwa gari.