Edwin Mtei
R I P
- Dec 13, 2008
- 181
- 342
Katika Taarifa ya Habari ya Channel 10 na TBC1 Meneja wa Kampeni wa CCM Abdulhaman Kinana amedai:
1. CHADEMA wamevunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu
2. Marando ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma
3. CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani
4. Ni vema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.
5. Mbatia wa NCCR-Mageuzi naye anadai vyama viongelee hoja na si Watu - Kuzindua Kampeni baada ya Ramadhani (Mfungo)
Nakubaliana na Mhe. Kinana kwamba Watanzania wengi si mabwege any more. Labda waliobakia mabwege ni wale wanaodhani sisi Watanzania hatujui kwamba CCM ikiongozwa na wale waliotajwa na Slaa pale Mwembe Yanga mwaka 2007 na waliotajwa tena na Mabere Marando juzi, walikwapua fedha za EPA na kuzitumia kwa Uchaguzi Mkuu wa 2005.
Nikiwa nimebahatika kuwa Muasisi wa hiki chama, na Mwenyekiti Taifa wa kwanza, natamka kwamba Jukumu kuu la CHADEMA na Mgombea wetu wa kiti cha u-Rais sasa ni kuelimisha umma wote juu ya ukweli wa UFISADI huu na kuwapa ujasiri wananchi wawakatae wale wanaodhani sisi ni mabwege.
HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!
Mimi sijui kama kuna kesi ya EPA dhidi ya CCM imefunguliwa. Ninachojua ni kuwa kuna individuals wamefunguliwa kesi.Marando ameituhumu CCM, so kwa vile hakuna kesi ya EPA dhidi ya CCM, matamshi ya Marando hayawezi kuathiri kesi zlizoko mahakamani ambazo haziihusu CCM. More particurlary kawataja Mkapa, Lowassa na JK, hawa hawana kesi iliyoko mahakamani. Ina maana hata JK asiongelee vita dhidi ya rushwa kwa vile kuna kina Mramba na Mgonja kesi zao ziko mahakani? Sijui huyu Kinana anafikiri kwa kichwa au anatumia nini. Huyo ndio manager wa kampeni wa kikwete, well, kweli sijui kama tutafika
=====
-Alihusikaje na EPA?
-Kwa nini aliamua kuwasemehe anaodai walirudisha fedha za EPA?
[S=4]Mkuu wa nchi kutajwa katika kashfa kubwa namna hii ukakaa kimya si salama hata kidogo. Akanushe na wanaomsingizia wapelekwe mahakamani. Mbona mgombea wa CUF Tanga amekamatwa kwa kumkashifu Kikwete? Mbona Mtikila yuko mahakamani akijibu tuhuma za kumkashifu?
[/SIZE]
Mimi ni mwanachama wa CCM , hili la kulia lia na kutojibu tuhuma linanipa wasiwasi kodogo.
Uongozi wa Chama Tawala unatakiwa ujibu tuhuma na si kuzifunika kwa maneno mazuri.
Tuhuma hizi vile vile ieleweke kuwa ni zinawahusu watu binafsi ambao wana uhusiano mkubwa na Chama, kwa nini watu hawa wasichukuliwe hatua?