Matusi au 'tuhuma' katika kampeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matusi au 'tuhuma' katika kampeni?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 29, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wadau, naomba nifahamishwe. ‘Matusi' ni nini katika medani hizi za kisiasa? Na nani mwenye mamlaka ya kutafsiri ‘matusi' katika kampeni hizi? Najua CCM wangependa sana kuwa watafsiri pekee wa neon hili.

  Hivi ‘matusi' aliyotoa Marando ya kuwataja vigogo wale wanne wa CCM anaowatuhumu kukwapua hela za EPA kutoka BoT ni matusi? Kwa tafsiri gani – ya Tido Mhando au tafsiri ya kamusi gani?

  Mimi nafikiri ‘matusi' kutokana na tafsiri ya Tido Mhando kwa mfano ni kwa Marando ‘kutaja majina' ya hao waliosuka mipango ya kuibia BoT. Na pengine kilichomkera zaidi Mhando ni namna Marando alivyowataja – kwa kujiamini kabisa – kusema kuwa hawatamfanya chochote kwani anao ushahidi wa kuwaumbua.

  Na hapa Tido Mhando asingetumia neno "matusi" wakati alipoongelea suala la kukata matangazo ya TBC hata kama yeye ndiye amejitwisha jukumu la kutoa tafsiri.

  Kwani neno sahihi hapa lilipaswa kuwa ‘tuhuma' au ‘madai' dhidi ya mtu mwingine ambayo hana ushahidi nayo. Kukimbilia kusema eti matusi ni mbinu tu wanaoitumia CCM katika kuzikabili hoja kama hizi.

  Mwaka 1996 katika mkutano wake wa kampeni wa kugombea Ubunge jimbo la Temeke, Augustine Mrema (wa NCCR wakati huo) alitoa tuhuma nzito dhidi ya rais Mkapa na viongozi wengine wa CCM kuhusu uchotaji wa hela Sh 900m/- kutoka serikalini. Sioni tofauti ya ile na hii ya Marando au na hata ile ya Slaa Mwembe Yanga ya 2007.

  Serikali ya CCM ilimshitaki Mrema kwa kutoa tuhuma za uongo, lakini kesi dhidi yake ilitupwa.

  Na ninamini bila chembe ya shaka kwamba jana Tido alipigiwa simu na mmoja kati ya vigogo wa CCM kumuamuru akate matangazo – kwani nina hakika baada ya kukaa BBC miaka kadha Tido anajua maadili ya profession yake na hivyo uamuzi huo haukuwa wake binafsi.

  Kwa CCM kuziita hoja, tuhuma, na madai madai wanayotoa wapinzani dhidi yake kwamba ni ‘matusi' hazikuanza jana. Nakumbuka wakati vyama vingi vilipoingia hawa CCM (hasa Wabunge) hawakuwa wamezoea kuzikabili hoja nzito za kukosolewa kutoka kwa wapinzani (kuhusu masuala hayahaya ya ufisadi na matumizi mabaya ya hela za umma) na hasa pale yalipokuwa yanaandikwa magazetini na kutokuwa na majibu nayo.

  Hoja hizo walikuwa wanaziita ‘matusi' kutoka kwa wapinzani. Nakumbuka katika kikao cha Bunge, Mbunge Ole Molloimet alilishambulia sana habari iliyokuwa imeandikwa katika Majira ikimnukuu Mrema kwamba ni matusi.

  Halafu Tido anasahu kuwa ‘matusi' aliyotoa Marando siyo mapya – yalishatolewa kule katika mkutano wa hadhara wa Chadema kule Mwembe Yanga mwaka 2007 ambapo Dr Slaa alipoitaja ile timu ya mafisadi 11, wakiwemo hawa wanne waliotajwa na Marando jana.

  Kitu ambacho CCM hawakukipenda ni jinsi TBC ilivyolazimika kuvipa fursa vyama vya upinzani nao kurusha matangazo yao – bila shaka kutoka msukumo na fedha za UNDP kama tunavyoelezwa.

  Ingekuwa ni yenyewe CCM ingeweza kuunda hoja kwamba TBC ni chombo cha umma kwa hivyo kisijiingize katika kutangaza mikutano live ya vyama vya siasa na kuongeza kwamba TV/Redio binafsi ndiyo zitumike kwa shughuli hiyo.

  Hapa wangewaweza wapinzani, kwani kwa kuwa CCM tu ndiyi ina mapesa mengi ingeweza kulipia coverage ya mikutano yao katika vyombo hivyo binafsi kitu ambacho vyama vingine vingeshindwa kutokana na gharama kubwa.

  Pili vyombo kadha binafsi ambavyo tayari vimeonyesha kuishabikia CCM – kama vile ITV, Channel 10 na Star TV vingeweza pia kukataa kutoa coveragen ya mikutano ya wapinzani kwani ni kitu cha hiari.

  Naweza kusema CCM inapenda kuona coverage ya kampeni zake zifike nchini kote na siyo za upinzani.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Naam!!!!!!!!!!
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tumewajua na kwa sasa kila chama kina haki yake
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Na kama hiyo ndio tafsiri yao ya matusi, basi watayasikia matusi mengi sana mwana huu maana nilimsikia Mbowe akisema yaliyosemwa jangwani ni rasharasha tu...
   
 5. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #5
  Aug 29, 2010
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani TIDO lazima afanye kazi TBC hata kama ni kujidhalilisha namna hii....Mimi namwona TIDO naye FISADI tu hakuna cha kupigiwa simu wala nini...NJAAA ZAKE tu
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 3,998
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa maoni yangu naona kitendo hiki alichofanya Tido Mhando kukatisha matangazo kwa madai kuwa yaliyokuwa yakihutubiwa ni 'matusi', kimempunguzia kwa kiasi kikubwa, hadhi ya umakini wake wa kiitaaluma. Nitakuwa muangalifu sana siku zijazo kumuweka mtu kama huyu kuongoza chombo cha habari cha taifa.
   
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Jamani naomba kuuliza kwani Tido alikuwa ana umakini gani? Huko BBC idhaa ya kiswahili alikuwa na cheo gani kilichomfanya a-qualify kuongoza TBC? au ni jina hilo la BBC ndo limemqualify? Mi tokea awali niliona kuwa uongozi wake hapo TBC ulikuwa ni wa kisiasa, ila aliweza kuyaficha makucha yake kwa mbwembwe mara kabadili jina kutoka TVT kwenda TBC, mara kaajiri vijana kama akina Taji Liundi lakini has there been any fundamental change? NO! Tusidanganyike .. Tido was who he is today always... but we are only realizing that today...
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Naona ilikuwa namna ya kijikosha,baada ya kuona aliyempa ulaji apo TBC nae yumo kwenye list ya marando
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,143
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  ccm ni wehu sana
  na mwaka huu watasikia matusi mengi sana
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  HUYO TIDO NAYE FISADI TU, ANGALIA TBC KINA MHANDO WANGAPI? DOES IT MEAN WANAE WALIKUWA WANASOMEA UTANGAZAJI, NA WOTE WALIPITA USAHILI TBC? :eyebrows:
   
 11. z

  zeeth Member

  #11
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kihivyoooo bwana maintain ur language,ccm foreva
   
 12. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2010
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona Makamba aliwahi kuwaita watu wehu na hatukusikia toka TBC kuwa ni matusi,Tido kafulia sio Tido yule wa zamani,kama alivyowa andika Johnson Mbwambo ,Tido sio yule wa zamani
   
 13. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 11,177
  Likes Received: 11,091
  Trophy Points: 280
  :becky::becky::becky: eheee ama kweli huu ni uhuru wa kuongea
   
 14. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 11,177
  Likes Received: 11,091
  Trophy Points: 280

  :smile-big::smile-big: haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 15. e

  emalau JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,101
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Huyo ndo tido kama alivyomwelezea Johnson Mbwambo, najua kwamba anajua kwamba his action is against his conscience
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 1,877
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 180
  Kachemsha,kazi za kupewa vilabuni madhara yake ndio haya,hana jipya.Arudie kutangaza mechi za mipira,lakini si kuongoza TBC.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Aug 29, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,934
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  Kama yaliyosemwa jangwani ni matusi, CCM au serikali wataenda kwenye vyombo vya sheria. Hata kama hawataenda huko basi wanawezafikisha malalmiko kwa magazeti yaliyoandika habari za mkuatano mbele ya MCT. Kama Ccm na serikali hawatachukua hatua basi ni wazi kuwa hayo hayakuwa matusi, na hapa ndipo Tido anatakiwa aeleze umma matusi ya jangwani ni yapi! Huyu Tido ametumia neno tusi ili ku sensitize jamii, ni sehemu ya kampeni za ''smearing''.
  Somo kwa vijana, unapotegemea mtu ili maisha yako yaenda mbele ujue utadhalilika, utapoteza heshima, utafungia taaluma yako kabatini n.k. Kila siku akili yako itakuwa ni kulamba miguu ya bwana ili upate mkate. Utahakikisha bwana anakuwa msafi hata kama uchafu huo unabaki mikononi mwako.
   
 18. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,698
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Katika Taarifa ya Habari ya Channel 10 na TBC1 Meneja wa Kampeni wa CCM Abdulhaman Kinana amedai:

  1. CHADEMA wamevunja maadili waliyosaini kwa kutumia lugha isiyo ya kistaarabu

  2. Marando ni Mwanasheria Kaongelea mambo ya EPA yaliyo mahakamani kinyume na Ethics za Taaluma

  3. CCM haiwezi kuongelea mambo yaliyo Mahakamani

  4. Ni vema kutumia lugha isiyo ya matusi ili hata baada ya uchaguzi viongozi waendelee kuongea pamoja badala ya kukwepana.

  5. Mbatia wa NCCR-Mageuzi naye anadai vyama viongelee hoja na si Watu - Kuzindua Kampeni baada ya Ramadhani (Mfungo)
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  True colors nyingi zitajionesha this tyme.
   
 20. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Mbatia ni CCM damu hivyo nothing special from him
   
Loading...