security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Tunaona ‘matunda’ ya urais wa Magufuli,
katu hatutaruhusu ‘mumiani’ wamkwamishe
Na Charles Charles
IJUMAA iliyopita, Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari, Balozi Ami Mpungwe alifichua mbinu chafu zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wa sukari nchini, kuificha bidhaa hiyo ili ionekane kuwa imeadimika kwa nia ya kutaka kumkomoa Rais John Pombe Magufuli na serikali yake.
Wiki tatu zilizopita, rais alipiga marufuku utoaji holela wa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi, badala yake akakabidhi jukumu hilo zima kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa asimamie kazi hiyo mwenyewe na siyo vinginevyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na makundi yaliyoshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu mwaka jana, Rais Magufuli aliainisha mambo mbalimbali ya kitaifa yakiwemo yanayohusu uchumi, ushuru, kodi na makusanyo ya serikali.
Akigusia tishio kwa viwanda vya sukari kuyumba katika uzalishaji kutokana kukosa soko la uhakika, ukwepaji wa kodi itokanayo na bidhaa hiyo kutoka nje pamoja na kusambazwa ovyo kiasi cha kusababisha inayozalishwa na viwanda vya ndani kuonekana inauzwa bei kubwa alimgeukia Majaliwa na kumwambia:
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, (kuanzia kipindi hiki ninapozungumza) hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje bila idhini yako”.
Lakini Ijumaa ya wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari, Balozi Ami Mpungwe alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameamua kuificha bidhaa hiyo kwa kuifungia kwenye maghala yao, lengo likiwa kutaka wananchi wamchukie rais kwamba agizo lake limesababisha sukari ikosekane nchini na kupanda bei.
“(Wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kwa taifa) wameanzisha kampeni ya kuwatia hofu wananchi wakiwaonyesha (kuwa) sukari imeadimika kutokana na agizo lililotolewa na serikali (kupitia kwa rais) la kudhibiti uingizaji wa sukari nchini”, alisema Mpungwe aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania huko Zimbabwe.
Mimi siyo mmoja kati ya viongozi, watendaji wala watumishi wa serikali na sina maslahi yoyote yale ya kifedha katika bidhaa hiyo inayoitwa sukari, lakini kwa namna zote ni mdau mkubwa wa bidhaa hiyo kwa sababu ni mlaji wake kama watu wengine.
Aidha, mimi pia ni mdau wa maendeleo ya uchumi, utamaduni, jamii na siasa za nchi hii, hivyo nina haki zote kwa kuzingatia Ibara ya 2(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inayosema ifuatavyo:
“Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo” (mwisho wa kunukuu).
Lakini katika upande mwingine, Ibara ya 11 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inaitaja rushwa kuwa adui wa haki, maendeleo na ustawi wa wananchi, hivyo ni moja kati ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania
na dunia nzima katika ujumla wake huku Ibara ya 12 nayo ikisema, na hapa ninanukuu:
“Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza serikali zake (mbili) kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma”.
Ikizidi kubainisha, ibara hiyo inaongeza kwamba CCM itazielekeza serikali zake hizo kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa serikalini na katika sekta binafsi, kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika kuzuia na kupambana na rushwa, kazi ambayo pia itaambatana na kuunda mahakama maalum itakayoshughulikia makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
“Sambamba na kupambana na tatizo (hilo) la rushwa, serikali pia zitatakiwa kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa umma”, inasema Ibara ya 13 ya Ilani hiyohiyo.
Watanzania sasa wanajua namna gani Serikali ya Awamu ya Tano inavyojitahidi kwa nguvu zake zote, kupambana na kero zote zilizokuwa zikiikabili nchi yetu ikiwemo rushwa iliyokithiri, zile ambazo waathirika wakubwa zaidi walikuwa ni wananchi wanyoge walio wengi huku matajiri wachache, watendaji na watumishi wa umma wasiokuwa waaminifu wakinufaika na jasho la wenzao.
Wanafahamu jinsi utumiaji mbaya wa madaraka na uozo ulivyokuwa umeenea katika maeneo mengi serikalini na taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jeshi la Polisi Tanzania (PT), Idara ya Mahakama, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pamoja na maeneo mengine mengi.
Wanaelewa namna gani wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu walivyokuwa mabingwa wa kukwepa ushuru na kodi za serikali, kuingiza nchini bidhaa zao kwa ‘njia za panya’, kusambaza na kuuza bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi yake au pengine zile ambazo zipo chini ya viwango au feki.
Wanajua namna baadhi ya watendaji na watumishi wa serikali na taasisi zake walivyokuwa wakitumia nafasi, madaraka au mamlaka waliyonayo kufanya kila aina ya ubadhirifu wa fedha ama wa mali ya umma, tena ambao walifanya hivyo bila wasiwasi wala kuhofia chochote kwa sababu ulikuwa umejengeka mtandao mpana unaofanikisha malengo yao ‘machafu’.
Walikuwa wamejipanga kwamba mwananchi asingeweza kushtaki au kusema popote kama kituo cha polisi, kusikilizwa na kuchukuliwa hatua kwa wahalifu, hivyo kuna wakati anayefanya hivyo kumbe alikuwa akisaidia kupanua mtandao huo wa wizi, ubadhirifu wa mali ya umma na hata vinginevyo.
Watanzania wanaelewa jinsi rushwa ilivyokuwa imefikia hatua mbaya kiasi cha kupelekea mpaka baadhi ya watendaji na watumishi wa serikali, taasisi zake au mashirika ya umma kuiomba kwa shinikizo, kuwalazimisha watu na hata njia nyinginezo na kusababisha mateso makubwa katika maisha yao ya kila siku.
Fikiria kwa mfano mgonjwa anapokwenda hospitali alikuwa akiandikiwa cheti na kuambiwa kwamba “hizi dawa hapa hatuna”, kisha anaelekezwa ama kuonyeshwa duka lililopo nje ya geti na kuambiwa aende akanunue hapo huku akitajiwa mpaka bei zake!
Lakini akisema fedha alizonazo kamwe hazitoshelezi dozi alikuwa akiulizwa kiasi alichonacho ili atafutiwe mahali pengine, ile ambayo hata hivyo ilikuwa ni ndani ya zahanati au hospitali ileile!
Fikiria kwa mfano wananchi walivyokuwa wakiuziwa na maofisa ardhi kiwanja kimoja watu watatu au zaidi, kisha wakifikishana mahakamani au sehemu nyingine ya kisheria, walewale waliotenda uhalifu huo wa jinai wanaangalia nani ana fedha kuwashinda wenzake na kuwasiliana naye mara moja ili ‘wamsaidie’ ashinde.
Hapo alitakiwa atoe rushwa na kuandikiwa hati mpya ya kughushi ili ashinde kesi, lakini pia ilibidi “azungumze lugha ya kueleweka” kwa watendaji wa mamlaka wa sheria iwe kwa hakimu, kwa mwenyekiti au wajumbe wa baraza la ardhi au mahali pengine, mianya ya uhalifu ambayo sasa imeanza kuthibitiwa kwa mapana yake yote.
Leo mwananchi anapokwenda ofisi yoyote ile ya umma kama idara ya afya, idara ya ardhi, idara ya usajili wa vizazi na vifo, idara ya sheria, kituo cha polisi, idara ya uhamiaji, idara ya elimu na kadhalika anapokelewa kwa namna zote zinazoitwa unyenyekevu, upole na kubembelezwa kwa lugha inayovutia na kuhudumiwa mara moja.
Ile kauli ya “njoo kesho” au “wiki ijayo” na kushindishwa benchi huku akipitwa kama haonekani sasa haipo katika ofisi zote za serikali. Hakuna tena mtumishi wa umma anayejibu wananchi kwa jeuri kuwa “faili lako halionekani ama “nisubiri kwanza”, na pia hakuna anayeomba wala kutaka apewe “pesa ya miwani” au “ya maziwa” kutokana na giza ama vumbi la masjala.
Hivi sasa tunashuhudia mpaka wakuu wa idara, vitengo au wa sehemu katika ofisi mbalimbali za serikali wakiacha viti vyao, kisha wanakwenda kuwauliza wananchi waliopo kwenye mabenchi kuhusu shida zao, zipo tangu lini na kujua endapo wameshasikilizwa na kuchukua hatua papo kwa papo.
Tumeshuhudia waganga wafawidhi au waganga wakuu wa zahanati, vituo vya afya na hospitali za serikali wakitoka ofisini na kwenda kusikiliza matatizo au kero za wagonjwa waliolazwa wodini, na pia wanafuatilia mara kwa mara huduma zote zinazopaswa zitolewe kama kwa wanawake wajawazito au pamoja na watoto wao.
Tumeshuhudia jinsi Serikali ya Awamu ya Tano inavyochukua hatua mbalimbali dhidi ya watendaji, watumishi na maofisa wake waandamizi wanapokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha, matumizi mabaya ya madaraka yao na kadhalika.
Wakati baadhi yao wakisimamishwa ili kupisha uchunguzi wa kitaalamu dhidi ya tuhuma zao, wengine wameondolewa moja kwa moja kutoka kwenye nyadhifa zao, lakini wapo pia ambao wamefikishwa mpaka mahakamani na kufunguliwa mashtaka.
Katika orodha hiyo, wengine walifanya makosa yao hadi miaka mitano iliyopita lakini wakaendelea na majukumu yao bila ya kuulizwa chochote, halafu kuna wengine waliotumia vibaya mamlaka waliyonayo na kisha wakapanda vyeo zaidi!
Nimejitahidi kwa namna moja ama nyingine kuonyesha, kukariri au kunukuu Ibara ya 11 – 13 za Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 kwa vile ni afisa mwandamizi wa chama hicho kilichopo madarakani, lakini nimefanya hivyo pia ili kuona endapo agizo la Magufuli la udhibiti wa vibali vya kuagiza sukari kutoka nje halina msingi ama anataka sifa.
Nimefanya hivyo ili kuthibitisha kwa ushahidi kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza kwa nguvu zake zote matakwa ya Ilani hiyo ya CCM, na pia inatimiza wajibu wake kwa kila Mtanzania ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005 inayotumika sasa inayosema ifuatavyo:
“Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria” (mwisho wa kunukuu).
Serikali inapopambana na uingizaji holela wa sukari kutoka nje ya nchi iwe kwa agizo la rais, makamu wa rais, waziri mkuu, waziri, naibu waziri, mkuu wa mikoa au mkuu wa wilaya; kudhibiti wizi, ubadhirifu wa mali ya umma au ukwepaji kodi inakuwa inatimiza matakwa ya Ibara hiyo ya Katiba ili kila mwananchi apate haki zake za kisheria.
Haiwezekani idadi kubwa ya wananchi hususan wanyonge kuona wakiteseka kwa kunyimwa huduma muhimu za kijamii kwa mfano matibabu mpaka watoe rushwa, kunyang’nywa umiliki wa mashamba yao, viwanja vyao au kulishwa bidhaa kama vile sukari, mafuta ya kupikia, unga wa sembe ama wa ngano, mchele na nyingine nyingi huku zimekwisha muda wake wa matumizi huko Ulaya, Marekani, Asia na kadhalika.
Haiwezekani kwamba serikali isiwadhibiti wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu ambao wanaingiza sukari kutoka nje ya nchi kwa njia za magendo, ukwepaji kodi na uovu mwingineo, hivyo agizo la rais kuwa kuanzia sasa ni marufuku mtu yeyote kutoa kibali cha kuagiza bidhaa hiyo kwa namna zote linalenga maslahi ya taifa.
Linalenga kuyalinda maslahi ya kila Mtanzania aliyepo Tanzania ama ya familia yake, ndugu zake na ukoo wake, yale ambayo kuna mengine yametajwa na Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo la 2005.
Katika hali hiyo yote, Watanzania wazalendo kama rais wetu katu hatuko radhi na tayari kuona wanaibuka ‘mumiani’ wachache kwa sababu ya uchu wao wa kifisadi, wizi wao ama uovu wao wowote na kutaka utekelezaji wa agizo hilo eti unakwama.
Hatupo radhi na tayari kuruhusu ‘matunda’ ya urais wa Magufuli ambayo sasa kila Mtanzania anayaona eti ‘yapondwepondwe’ na kundi hilo la ‘mumiani’.
Tunataka watuelewe kwamba hatutakubali hata siku moja kusujudia uovu wao wa kutaka waendelee kuuhujumu uchumi wa taifa, kujilimbikizia mali ama fedha kwa njia chafu na hata vinginevyo.
Ndiyo maana sikushangaa kwa mfano kuona asilimia 82 ya watazamaji walioijibu swali la Kipima Joto la Kituo Huru cha Televisheni (ITV), Jumamosi iliyopita lililohoji kama wanaoficha sukari kwenye maghala yao ili aidimike wachukuliwe kuwa wanahujumu uchumi wakikubali kwamba “Ndiyo”.
Endapo wanadhani watafanikiwa kwa hakika watakuwa wanapoteza wakati wao bure kwa vile Watanzania wengi wanaunga mkono agizo la rais, hivyo waliokuwa wamezoea kutajirika kwa kutumia kichaka hicho hivi sasa wakubali kuwa “imekula kwao”.
Assalaam Allekhum Waramaturah Wabarakhaty!
Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Itikadi na Uenezi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0787 088 870