Matumizi ya nyaraka za ofisini kama vifungashio madukani yadhibitiwe

Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
4,628
6,563
Wadau, kwa muda sasa nimekuwa najiuliza kuhusu uhalali wa nyaraka mbalimbali za kiofisi kutumika kama vifungashio vya bidhaa mbalimbali madukani kama ambavyo wengi wetu tumepata kushuhudia.

Mara nyingi unakuta karatasi zilizotumika kutengenezea vifungashio hivyo zina majina ya watu na taarifa nyeti sana za ofisi, watumishi au wadau binafsi. Mfano jana nilinunua bidhaa fulani na nilipofungua karatasi ya kifungashio ikawa inahusu course field report moja ambayo title yake ilikuwa ni "Waste and Surface Water management in Central Business District (CBD) of Arusha Municipality". Hii ilikuwa ni field report iliyotoka kwa wanachuo watano waliokuwa wakisoma pale UD (faculty of arts and social sciences-Geography dept). Katika yale majina matano niliweza kutambua jina la jamaa yangu mmoja hivi wa karibu. Na pia kutokana na ukubwa wa karatasi niliweza kusoma japo sehemu ya kurasa chache za report yao. Hii nimeitoa kama uthibitisho tu wa kile nikisemacho lakini kuna makaratasi mengine mengi tu yanakuwa yanahusu demotion au promotion za watumishi, mikopo ya watumishi kazini, barua za onyo kwa watumishi n.k, mitihani yenye kuonyesha kabisa matokeo ya ufaulu au kufeli kwa mwanachuo n.k. ambayo ni mambo yanayotakiwa kuwa siri siku zote.

Mimi ninavyoona badala ya hizi nyaraka kuwa disposed of kwa njia ya kutupwa kiholela, kugawiwa bure au kuuzwa kwa watu basi ziwe zinafanyiwa re-cycling au ziteketezwe kabisa ili kulinda usiri wa ofisi na watumishi wake au wadau wake wengine. Na wakati wa kufanya total destruction ya hizo nyaraka kuwepo na usimamizi wa uhakika. Nawasilisha ili kupata michango yenu wakuu.
 
Back
Top Bottom