Matumizi mabaya ya madaraka: Wafanyakazi 11 wa TRL kufikishwa mahakama ya Kisutu leo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa TRL (Tanzania Railway Limited) watapelekwa Mahakamani Kisutu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na nyaraka, ikihusiana na manunuzi ya behewa ya kokoto.
 
Yaani kipindi cha mkwere kuna watu walikuwa wanajenga nyumba ya ghorofa hata nne ndani ya mwezi mmoja. Ndio hawa majipu sasa
 
Yaani kipindi cha mkwere kuna watu walikuwa wanajenga nyumba ya ghorofa hata nne ndani ya mwezi mmoja. Ndio hawa majipu sasa
Yule mama Chuwa alipodai kwamba alitonywa kwa SMS toka juu kwamba Waziri mkuu anakwenda kumtembelea, aweke mambo sawa na kupelekea kutaka kumdanganya Waziri mkuu kwa kuwasha pump ambayo haijafanya kazi kwa miaka mitano mizima, kiasi cha kupelekea serikali kuibiwa Mabilioni na wajanja, huku Mama Chuwa na aliyemtumia SMS wakiwa wanalijua hilo miaka yote pasi na kuchukua hatua, Je huyo aliyemtumia Mama Chuwa hiyo SMS ni nani? Na kuna sehemu ngapi ambazo madudu bado yanaendelea ni mpaka atakapokwenda kutembelea Waziri Mkuu ndio ayabaini? Na sehemu ngapi ambazo Waziri Mkuu ameshazugwa kwamba hali ni shwari kumbe ni mwendo wa SMS ndio unaotumika siku hizi?
 
Ee Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania na watu wake ktk kutenda haki ili watanzania wote wafurahie kuwa watanzania.
 
Brigadea u nadhani Magufuli anaweza kujivua nguo kwa kumtimua Profeser Muongo
Subiri sana
 
MWIGULU NCHEMBA ATEMBELEA MACHINJIO YA MAZIZINI,UKONGA KWA KUSHTUKIZA USIKU NA KUKUTA NG'OMBE ZAIDI YA 400 KUCHINJWA BILA VIBALI,HIVYO KUKOSESHA SERIKALI MAPATO.
 
Nina imani na Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli. Nashanganzwa na watu walioaminiwa na yeye kila siku wanakutwa na madudu ya kuhujumu uchumi. Jamani mnataka nini kama hamuoni juhudi za rais. Tafadhali rais funga hao watu maana hawana shukrani.
 
Alafu Rais wetu wazungu wanamuuliza swali simple kama hili ;kwanini nchi yako ni maskini ??
anashindwa kulijibu !!!!
 
Mh. Rais anatakiwa "Amfukuze kazi Prof. Muhongo Haraka sana" kwa kosa la kuihujumu serikali yake na kutokuwa mwaminifu kwa kiapo chake mbele ya rais.
Kama kweli alituma hiyo sms basi ndio hiyo red handed yenyewe. Ya kutaka kujua sababu yatakuja baadaye.
 
YETU MACHO NA MASIKIO....paka akiondoka panya hutawala.Jk amestaafu viwavi wake wanapiga deal!
Magu kunjua makucha haraka.Mchelea mwana kulia.......
 
Back
Top Bottom