Matokeo ya NECTA

Samedi Amba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
227
Reaction score
178
Habari wadau,
Matokeo ya darasa la saba tayari. Hongera kwa waliofuzu. Kwa wale ambao mambo hayakuenda yalivyotarajiwa, hamna haja ya kukata tamaa. Kuna njia nyingi tu za kumuua panya...

Bila ya kupoteza muda nitaenda kwenye concern yangu kuu. Leo, kuna mdogo wangu alikuwa anatarajia matokeo. Sasa kwa vile kijijini hamna internet ya fasta kihivyo, nikaombwa nifanye the necessary. Nikaingia mtandaoni nikafanya ya kwangu na kutoa mrejesho.

Nikajiuliza hakuna njia rahisi ya kupata matokeo? NECTA hawana SMS system ambako mtu anaquery na kupata matokeo. Kwa mfano, nikiandika neno PS1029000-100 kwenda 200500 siwezi nikapatiwa results hapo hapo? Nawaza tu kwa sauti...
 
Hivi daraja D ndio umefeli si ndio[emoji53][emoji53]

Nina kitoto nakikuza hapa nimeangalia matokeo yake kina D
 
Hivi daraja D ndio umefeli si ndio[emoji53][emoji53]

Nina kitoto nakikuza hapa nimeangalia matokeo yake kina D
Hujafeli mkuu. Matokeo ndo mabaya. Huwezi kufeli maisha kisa mtihani
 
Mhhh D naona kazingua na hata akipata chance yakwenda secondary basi second selection...
Hivi daraja D ndio umefeli si ndio[emoji53][emoji53]

Nina kitoto nakikuza hapa nimeangalia matokeo yake kina D
 
Mhhh D naona kazingua na hata akipata chance yakwenda secondary basi second selection...
Kamefeli sawa na division 4 [emoji23]mkuu hana pakwenda sema atapata cheti cha kuhitimu darasa la saba [emoji16][emoji16]nina katoto kama mama yangu mdogo yaani kamegonga vzr haswa ..
Kiswahili - A, English - C, Maarifa - C, Hisabati - B, Science - C, Average Grade - B [emoji4][emoji4][emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…