"Mateja" Zanzibar wadai "Unga" umeadimika

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Bei ya madawa ya kulevya visiwani Zanzibar imeendelea kupanda kwa kasi huku biashara hiyo ikifanyika kwa siri na tahadhari ya hali ya juu, kutokana na hofu ya kukamatwa na vyombo vya dola vilivyoanzisha mapambano maalum dhidi ya matumizi ya mihadarati hapa nchini.

Camera ya Channel Ten imetembelea katika maeneo mbalimbali yaliyoshamiri matumizi ya dawa za kulevya na kushuhudia hali halisi inayoendelea hivi sasa tangu Serikali zote mbili zilipoamua kulivalia njuga suala hilo la mihadarati.

Wakizungumza na Channel Ten, baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya wameipongeza Serikali kwa kuamua kupambana kwa vitendo dhidi ya watu wanaofanya biashara hiyo ambao wanaangamiza mamia ya vijana pamoja na wanawake na kupoteza nguvu kazi kubwa ya Taifa.

Watumiaji hao wa dawa za kulevya wamesema wapo tayari kuachana na matumizi ya mihadarati na kuiomba Serikali kubeba gharama zinazotozwa katika vituo maalum vya kurekebisha tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nhunga Juma Mihayo amesema Serikali imeviachia vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wale wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
 
Wasaidiwe matibabu hao ambao wapo tayari kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya,
Kwa kufanya hivyo hapo Serikali itakua tayari inapigana vita kwa njia nyingine ya kuwapunguzia wateja/watumiaji/wanunuzi hao wauzaji wa hayo madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom