Matapeli katika mitandao ya kijamii kwa kudukua account

ASIE NA MAKUU

Member
Aug 10, 2021
40
65
Habari za asubuhi wanabodi.Ngoja niende moja kwa moja kwenye hoja kama inavyojieleza hapo juu.
Siku za karibuni kumekuwa na kadhia ya mashambulizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook.Nimeshuhudia baadhi ya marafiki zangu wakiwa wahanga wa kadhia hio.

Wanadukua account kisha wanaposti kuwa umepata promotion kutoka katika UNICEF,WORLD HUMATNIARION SUPPORT ,GRANTS,WFP N.K.

Tena wanascreenshot kiasi ulichotumiwa ili uweze kuwavuta wengine nao wajiunge kwa kugusa link ambayo itakupeleka Watsap.

Na walivyojipanga baada kuhaki account yako wanakimbilia sehemu ya kukoment ,kila mmoja anaekoment anashukuru kuwa kapata hela nyingi muda mchache baada ya kutoa kiasi fulani cha pesa kama kianzio kisichozidi laki 3 na nusu.

Nawakumbusha hao ni matapeli ,hata kama una rafiki unaemfahamu ukakuta account yake imepostiwa ujumbe huo ni bora umpigie kama una namba yake kujiridhisha.

Na hao matapeli ukiangalia code wanazotumia ni za kutoka Kenya.
TCRA tunaomba muingilie kati kulinda faragha zetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom