Matajiri wengi wa Tanzania hawako wazi njia walizotumia kufika mafanikio....kwanini???

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Tofauti sana na wenzetu wa Ulaya na America matajiri wanajivunia sana utajiri wao na njia walizopitia kupata utajiri huo kiasi cha kuandika hata vitabu vya namna ya kupata mafanikio.

Lakini ni tofauti sana na huku kwetu MTU akishakuwa tajiri tu basi ni ngumu sana kueleza jinsi alivyopata huo utajiri na ukitaka kugombana naye basi Karibu kudadisi hata alipataje huo utajiri.

Matajiri wengi wa kwetu wanapenda watu kuendelea kuwa masikini au?

Kwanini wengi hawasemi njia walizopitia kufika utajiri huo??
 
Mkuu hebu tupe orodha ya hao matajiri unaowasema, na kwa nini mtu asimame hadharani atangaze njia alizotumia kupata utajiri!? Ulaya na Amerika ya wapi ambapo hao matajiri husimama na kutangaza jinsi walivyopata utajiri wao zaidi ya sisi kusoma baadhi ya vyanzo vya habari jinsi walivyopata huo utajiri, na mara chache sana matajiri wote kuandikwa zaidi ya wale maarufu. Ndo nyinyi mkiona mtu kainuka ndo mnaanza kuhoji, wakati akiwa chini hamkuhoji
 
Tofautisha tamaduni za Africa na ulaya

Jiulize kwanza ma profesa wangapi wamechapisha vitabu then uulize kwa matajiri

Mimi naona wa Tz hatuna utamaduni huo na muamko huo wa kuandika vitabu,ku expose,

Lakini mbona wapo kama sabodo ameandika vitabu mbalimbali,nakala

Sabodo kinachombeba ni elimu tofauti na matajiri wengine
 
》Laws of nature..binadamu tumeumbwa tufauti.. pia tuna utamaduni tufauti, btw hata wakiandika vitabu, sisi wabongo ni wavivu kusoma...

》Na hata ukivisoma, ukute njia alopitia kuzipata hizo mali,ukiitumia ww unazidi tu kuwa masikini.. (circumstances n timing)
 
Si jambo jema kila mtu kufahamu historia ya maisha yako.
Kwa maana wapo wabaya ambao wakijua wanaweza kutumia nafasi hiyo kukuangamiza ama kukushusha chini.
 
Tofauti sana na wenzetu wa Ulaya na America matajiri wanajivunia sana utajiri wao na njia walizopitia kupata utajiri huo kiasi cha kuandika hata vitabu vya namna ya kupata mafanikio.

Lakini ni tofauti sana na huku kwetu MTU akishakuwa tajiri tu basi ni ngumu sana kueleza jinsi alivyopata huo utajiri na ukitaka kugombana naye basi Karibu kudadisi hata alipataje huo utajiri.

Matajiri wengi wa kwetu wanapenda watu kuendelea kuwa masikini au?

Kwanini wengi hawasemi njia walizopitia kufika utajiri huo??
Dangote vipi,umeona kitabu chake? Najua baadhi huandika,ila huachia familia zao .
 
Nakubaliana na sababu ya njia zilizotumika kupata utajiri. Vilevile kuna tatizo la wivu mbaya. Watu wengi wakitajirika wanaongeza maadui kwasababu ya wivu kwahiyo hawaoni umuhimu wakueleza mbinu walizotumia kwa maadui zao
 
Ukimwambia tu mbongo njia zako anakimbilia kwa mganga na majina yako matatu.ukiwa kazini unabanwa usiwe na kipato mpaka mtu anaamua atumie njia mbovu za kufanikiwa na anakuja kukosa maneno sahihi ya kukuekeza jinsi alivyofanikiwa,maana aliiba mafuta ya office,aliiba stationals,alipiga kila aina ya magumashi,per diem hewa.so kukwambia njia zake wala hawezi na akiwa mhalifu wa kupitiliza sehemu ya kazi anaweza kuja kushindwa hata kukwambia hela aliyonunulia gari aliipataje maana ina figusu nyingi mpaka yeye mwenyewe kajisahau alipataje.anakwambia eti ni MUNGU tu ndugu ndo alinisaidia
 
Kwa waganga na majina yako Matatu!!!!!!! Mmmmh kazi IPO aiseee!!?!!
 
Si jambo jema kila mtu kufahamu historia ya maisha yako.
Kwa maana wapo wabaya ambao wakijua wanaweza kutumia nafasi hiyo kukuangamiza ama kukushusha chini.
Na huko majuu why wako proud na mafanikio yao na njia walizopitia??
 
Ujue ili iweje? Tatizo wengine ni wivu tu unaowasumbua. Tumia na ww njia zako ili ufanikiwe
''kazi kujadili utajiri wa wengine tu''
TAFUTA VYA KWAKO NDIYO UTOLEE UZI. TATIZO LA MASKINI BADALA AFANYE KAZ YY KAZI YAKE KUJADILI MATAJIRI TU
Kama amepata kwa nguvu za giza ww inakuhusu nn? MATAJIRI HAWANA TIME KBSA NA MASKINI LKN CHA KUSHANGAZA MASKIN NDIYO ANAPATA MUDA WA KUTUJADILI.
 
Back
Top Bottom