Jamal Malinzi
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 710
- 650
- Thread starter
-
- #881
ikizu waamuzi hawabadilishwi bila sababu ya msingi na si kila maamuzi tutakuja kuyatolea ufafanuzi jf.Mkuu wa mpira hapa Nchini Tanzania.
nilikwambia kwenye ushauri wangu na maswali kwako hatimae yametimia.
KWANZA
Kuhusu suala la kubadilisha waamuzi wa mechi za TOTO ukakanusha sijui na la mechi ya jana ya TOTO na GEITA utalikanusha? aibu aibu sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwako kama mkuu wa mpira jitafakari kwa hilo.
PILI
Kituko kingine ni hiki kilichotokea kwenye kamati yako ya utendaji ni juu ya uuandaji wa kamati ya kuwa inashugulika na adhabu hili umelitoa wapi mbona kwenye katiba halipoooooooo jamani huna washauri au husomi katiba ya tff ni aibu aibu na shidaaa hao watu watamuhukumu nani na kwa misingi ipi? na hizo kamati zako za kutoa haki zitafanya kazi gani ikumbukwe fifa masuala yaote yanayohusu adhabu kuna kamati huru zilizojaa wanataaluma wewe kumchagua kalia na yahaya wawe mahakimu hilo umelitoa wapi? kumbuka utakuwa RAIS bogasi kuliko wate waliowahi kuongoza soka la bongo.
TATU
INAUMA sana kusikia nawe unajihusisha na mpango mchafu wa kuhakikisha toto anaingia ligi kuu RAIS jitafakali wapi ulipoanguka na kama hujui nambie niendelee kukusaidia kwa ushauri, Timu ya TOTO mechi 7 zote ilizocheza zimetokea vurugu au mpira kutoisha umewapa point ni aibu
ikizu waamuzi hawabadilishwi bila sababu ya msingi na si kila maamuzi tutakuja kuyatolea ufafanuzi jf.
TFF ikiamua kuwa inaunda kamati au kutekeleza maamuzi yake kwa kuangalia nani yanga/simba/azam/mtibwa/ndanda/coastal etc basi hatutakaa tufanye maamuzi kwenye mpira wa nchi hii.Mathalan wenyeviti wa hizi kamati wamekugusa,niambie ni maamuzi gani wameyatia ambayo wewe unayaona ni yanaegemea upenzi wao wa klabu.
Kwenyenhili la kuunda kamati ya uendeahaji wa ligi,hii kamati ni kamati NDOGO ya bodi ya ligi na tangia BODI ianzishwe siku zote imekuwa ikisikiliza na kutoa maamuzi kwa masuala ambayo ni NON APPEALABLE na hii mandate Bodi imepewa na kanuni za BODI ya ligi ambazo uongozi wangu umezirithi toka awamu iliyopita.Kamati ya utendaji ya awamu iliyopita ndiyo ilitengeneza kanuni hizi,mbona ulikuwa hujawahi kulalamikia hilo.Malinzi kuboresha utaratibu ambao tayari ulikuwepo imekuwa nongwa?
Washindi watapewa zawadi zao muda si mrefu na jezi kuzinduliwaMheshimiwa Jamal Malinzi, hadi leo hii tunangoja kujua jezi mpya ya Taifa Stars.
Kila tumikia simu huko offisini tunaambiwa.. ngoja tutatangaza... Tuambiane sasa tusuburi hadi lini?
Tupatie kauli isiyo tata.!
hivi raisi,hili swala la kuongeza wachezaji wakigeni wafike hata 10 linafanyiwa kazi kwenye..!?
maana hawa wachezaji wakibongo wanaturudisha nyuma sana hususan kwenye virabu vyetu hivi..
Kimbunga mwisho wa siku Watanzania wanachotaka ni kuona matokeo mazuri uwanjani.Swali ni je sisi kama nchi tunawekeza kiasi gani kuhakikisha timu zetu za vijana ambazo ndilo chimbuko la Taifa na Twiga stars zinafanya vizuri.Mtihani mkubwa uko hapo.Mkuu Jamal Malinzi ni muda kiasi umepita tangia uchukue hatamu za Urais kukiongoza chama chetu cha mpira wa miguu. Je tangia uchukue madaraka hayo hadi sasa ni mafanikio gani ambayo unaweza kuwaambia watanzania wapenda mpira kwamba umeyapata ndani ya muda wa uongozi wako hadi leo hii?
Pili, bila shaka kuna changamoto ambazo umekumbana nazo tangia umeingia madarakani ikiwemo kushutumiwa kuwa wewe ni mkabila na pili una uyanga; je hadi sasa ni changamoto gani ambazo unaona zinakukwamisha kufikia malengo yako na unazikabili vipi hizo changamoto?
Kimbunga mwisho wa siku Watanzania wanachotaka ni kuona matokeo mazuri uwanjani.Swali ni je sisi kama nchi tunawekeza kiasi gani kuhakikisha timu zetu za vijana ambazo ndilo chimbuko la Taifa na Twiga stars zinafanya vizuri.Mtihani mkubwa uko hapo.
Kitulo na wakimataifa mabadiliko ya ratiba mara nyingi yanatokea tokana na matukio mbali mbali mfano matakwa mahsusi ya timu ya Taifa au vilabu vinavyoshiriki michuano ya Afrika.Nikupe mfano,mwaka huu 2015,Tanzania tutashiriki qualifiers za CHAN,AFCON na World cup Russia.CHAN na WC qualifiers tutaanzia mtoano.Ratiba ya ligi kwa vyovyote vile itategemea tuta progress vipi katika knock out hizi.Hali kadhalika kwa Yanga iliyo kwenye mashindano ya Afrika.Wengi wanasema mbona Ulaya hawabadilishi ratiba,hao wanasahau kuwa wenzetu miundo mbinu yao inarahisisha usafiri na size ya nchi zao nyingi ni ndogo kulinganisha na Tanzania hivyo ni rahisi jumatano kucheza Ufaransa na jumamosi ikacheza Manchester.Sisi ukicheza jumamosi Tunis ndo basi tena wiki kwenye ratiba imepotea hiyo.
Mfano mechi ya away confederation cup Yanga watacheza kilomita zaidi ya mia moja nje ya Bulawayo Zimbabwe,watoke hapa waende Harare waruke kwenda Bulawayo,waendeshe gari kwenda uwanjani mgodini watarudi lini nchini kucheza ligi?