faiza do you know how much i am worth mpaka ufikirie kukagua mali zangu?
Nikusaidie Faiza,Federation nyingi Africa zinaendeshwa kwa nguvu na uwezo wa viongozi wa hivyo vyama,Look at Zimbabwe FA Mozambique FA etc FA presidents wao ndil wanahangaikia timu hasa za vijana.Kwa nini hujiulilizi majuzi bila udhamini wa uhakika tuliwezaje kuingiza kwenye mashindano ya Africa timu mbili za wanawake under 20 na senior,tukaingiza wavulana under 17 na under 20?Na zote zilikaa kambini zikala zikalala zikapanda ndege kwenda lusaka,lagis,nairobi na jburg.Taifa stars imekaa kambini since march hadi august inakula,inalala,posho,kambi botswana na timu haidai posho,Faiza bado una fikra potovu kuwa Malinzi mwizi? FIFA's motto ni "fair play".
maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo
Kipaji Halisi hili la Yanga na cecafa siai kama federation we tried our best kuokoa situation na hili Yanga wanajua,walichoamua cecafa ndo hicho.
komeka we acha tu,ahsante kwa kulitambua hilo.Ifikie wakati vilabu (hasa hivyo vinavyoitwa vikubwa) vitambue kuwa in thw long term kutafuta ubingwa wa papo kwa papo kwa kutumia wachezaji wa nje hakuwasaidia,kuwekeza kwa vijana ndio nguzo ya mpira wa nchi yoyote duniani.
uanachama wetu cecafa ni wa kisiasa na kihistoria kuanzia enzi za Gossage tukipigania uhuru.Mwaka huu tuliwaomba cosafa watualike nafasi ikawa ngumu (wamealika Ghana ).Hata hivyo usidhanie kote ni shwari,changamoto za uongozi ziko kila mahali,ni kukabiliana nazo tu.
Kisiasa, kiuchumi na kihistoria tuko vizuri zaidi na nchi wanachama wa COSAFA kuliko CECAFA. Naamini unazikumbuka nchi 5 zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Africa. Naamini pia unakumbuka uwepo wa miundo mbinu kama TAZARA, TAZAMA, Malawi Cargo, UMOJA bridge etc. Mwisho naamini pia unakumbuka vyama kama TAMOFA. Sasa kwa kuwa CECAFA wanaingiza siasa katika mpira na sisi tunataka kukuza mpira wetu tuwaambie finito! Usishangae huenda kuna mkono wa Kagame kuenguliwa kwa Yanga eti kwa vile JK ni shabiki wa Yanga na kwamba JK na Kagame haziivi! Ha ha haaa!
Twende COSAFA kwa ndugu zetu wa ukweli ambao hawana longolongo kama za Musonye.
Watanzania watu wa ajabu sana, kwa hiyo leo mnataka kusema matatizo ya soka la bongo yanasababishwa na musonye au kuwa cecafa?
wewe unaonaje kwan kama mna programe zenu halafu mtu mwingne anakupangia kuanzia kocha mpk wachezaji kuna nini hapo. Jamal Malinzi wewe kama raisi hili linahitaji ufafanuzi wa kwa wananchi na wadau maana rumours zpo nyingi kuhusu suala hili la yanga kuna hyo ya kupiga hela toka AZAM pia kuna hyo ya beef kati ya musonye na YANGA pia kuna hilo la ushabiki wa JK kwa YANGA ndo umeponza. huwezi ukasema maji yameshamwagika halafu basi je na mie nikichoma moto uwanja wa karume kisha nikasema yaishe maji yameshamwagika nitaeleweka. Jamal Malinzi hebu tunza heshima yako katika hili kwa kulitolea ufafanuzi hata kama sio humu basi katika media nyingne. nakuamini bado unaweza ila hili la yanga cjakuelewa hata kidogo
Katika hilo la rushwa tuko pamoja ndugu ya blueband,tetesi za azam kwenda kagame hv,plan A kuna bloger mmoja aliripoti kuwa azam amepewa nafasi ya km mualikwa ktk yale mashindano,hiyo ikaonekana ni kuvunja kanuni ya cecafa kwani nchi mwenyeji ndio inaruhusiwa kuwa na timu mbili,plan B barua ya mualiko ilikaliwa pale tff mpaka Yanga waliposema hawajapata barua plan C ikakubali dhamira ya wapigaji,ndio maana hapa tunaambiwa maji yashamwagika,kwa mfumo huu na kwa watu km hawa bado sana kwa sisi kupiga hatua ktk soka
Haya mambo ya cecafa tungeachana nayo coz ni upuuzi tu ... Makoyematale naona umekomalia cecafa utadhani ni mashindano ya klabu bingwa africa wakati ni upuuzi Wa musonye na wenzake isiitoshe cecafa haina mchango wowote kwny soka letu
Malinzi
Katika muda mfupi tu wa uongozi wako unakabiriwa na tuhuma nyingi nzito. ili kusafisha jina na heshima yako, unaonaje iundwe tume ambayo ni independent na ina watu wenye heshima kama waakili Said El Maamry, ili kuchunguza na kuweka bayana hizi tuhuma hapa chini
1) Saga la Azam lilivyogubikwa na mwendo wa rushwa, ili ishiriki kombe la kagame kwa mlango wa nyuma. kwani hapa zimeshushwa detail nyingi.
2) Tuhuma za wewe kuweka watu hotelini, na kuwalipia wakati wa uchaguzic.c @FF
3) Kuhamisha offisi kinyemela na kuiweka taasisi ya TFF katika wakati mgumu ki pesa
4) Mradi wa maduka (frame)
5) Kushiriki kumtorosha kinyemela Ngassa kwenda kufanya majaribio Afrika ya Kusini, bila kuwashirikisha Yanga. Habari hizi zilikaliliwa na blog moja , mwenye blog aliandika kuwa mlikutana uwanja wa oliver Tambo, ukawa unalalamika kuwa umefanya kazi kumleta sasa Yanga wanafanya nini? Hili swala halitakiwi kufanywa na mtu kama wewe, inawezekan, huyu mwandishi anataka kukumaliza, au wewe mwenyewe hujajua miiko ya kuongea na wandishi wa habari
Nia si kukutafuta ubaya, bali ili kusafisha jina lako na heshima yako, na taasisi kwa ujumla.