Kipaji Halisi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 2,280
- 1,366
Ni udhaifu pia wa uongozi wa TFF. 'Mtu akikuambia jambo la kipumbavu, nawe ukalikubali, anakudharau' (J. K.Nyerere, n.d.). CECAFA wamewaambia jambo la kipumbavu TFF kuwa Yanga hawana sifa ya kushiriki mashindano eti kwa sababu wanapeleka kikosi B huku TFF wakijua fika kuwa wale ni wachezaji halali wa Yanga. Kwa kitendo cha TFF kukubali upumbavu ule, CECAFA imewadharau kana kwamba TFF haina viongozi ndiyo maana CECAFA iliwataka TFF wawaandikie barua Yanga na wao kukaa pembeni nje ya tatizo. Nashangaa ni kwa nini viongozi wa TFF hawajaomba radhi hadi sasa kwa kukubali upumbavu ule. CC. Jamal Malinzi (Mkuu una utetezi gani katika hili?).
J .Malinzi huwa unapita jf naomba jibu tff ni mwanachama wa fifa.je iweje tff iwe mwanachama wa chama ambacho sio mwanachama wa fifa? chama chenyewe ni cecafa
la pili yanga ilipeleka majina kwenda kagame cup na hayo majina tff mliyathibisha je hayo majina yalikuwa sahihi
tunaomba majibu ya kina
Hili ni swali kutoka kwa mdau #mansoorsaid ameliuliza katika thread nyingine, nimelileta huku kwako mkuu. Lipo hivi
"J .Malinzi huwa unapita jf naomba jibu tff ni mwanachama wa fifa.je iweje tff iwe mwanachama wa chama ambacho sio mwanachama wa fifa? chama chenyewe ni cecafa
la pili yanga ilipeleka majina kwenda kagame cup na hayo majina tff mliyathibisha je hayo majina yalikuwa sahihi
tunaomba majibu ya kina"
hawa Dama city toka somalia ni zaidi ya timu B...hamna kitu..pia mbn APR nayo imejaza makinda.. Makoye nimekusoma vzr
Asante Mkuu kwa kunisoma, ningependa kuona jambo hili halipiti hivi hivi, viongozi wa TFF waliohusika katika hili wachukuliwe hatua. Siyo lazima wafutwe kazi wanaweza kuandikiwa barua za onyo kuonesha kuwa walichokifanya ni upumbavu mtupu.
Kwa kuongozea tu...tenga km mwenyekiti naye ameruhusu tu hili...kayuni ni mjumbe wa kamati tendaji naye kimya...ktk kagame hii APR inawachezaji karibu nusu nzima ni under 17 lkn wameruhusiwa..
wakuu unajua musonye ana shida na yanga muda mrefu tu toka yanga walipokataa kuingiza timu kucheza na simba mwaka ule na kuanzia hapo amekua akiwaundia zengwe sana. pia tff bila kujua wameingizwa mkenge na wao wakaingia kama yanga ilikosea waliotakiwa kuwajibishwa ni tff kwa kuyapitisha majina hayo
sikupati nifafanulie jinsi ya kukupataMajuzi Hollyman alifungua thread ya aina hii.Nia na lengo lake lilikuwa ni zuri,namshukuru.Nimeamua nifungue mwenyewe hii thread ili iwe ni uwanja wa kudumu wa kuniuliza maswali,kutaka ufafanuzi na pia kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya mpira wetu.Kwa ruhusa ya moderators ninaomba uwe ni ukurasa wa kudumu hapa jf.
Jamal Malinzi
Rais wa TFF
Dar es salaam 04/Feb/2014
Kweli kbs..musonye haipendi yanga na anajionesha dhairi shairi..nasikia anaondoka mwaka huu
Kweli kbs..musonye haipendi yanga na anajionesha dhairi shairi..nasikia anaondoka mwaka huu
Mr prezidaa tunahitaji majibu ya vigezo vilivyotumika kuitoa Yanga ktk mashindano ya kagame
Dah!kaukimbia uzi aliounzisha mwenyewe!
Kuna umuhimu hii link kuwepo? moderator (Muheshimiwa Invisible) funga hii link, ni dhihaka na dharau ya juu kwa watu, huwezi kuwa unakuja kujibu ukishangiliwa tu kukiwa na swali kinyume una sepa. maendeleo huletwa na mawazo tofauti.