MKALIKENYA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,196
- 486
Sera hii ya Jamal Malinzi na wenzake akina Mayanga HAIJAWAHI kuwepo duniani na inaanzia TZ!Sijapata ona popote duniani nchi ikaendelea kisoka bila kuwekeza!Kama issue ni vijana kuna vijana wengi wanacheza soka la hali juu league zetu!Hawa wa mitaani wameandaliwa lini,wapi na nani?
Tunacheza na Zimbabwe kufuzu mataifa huru baadae mwezi ujao tutegemee kipigo kikali!
Malinzi kashindwa kazi akae miaka yake 4 aondoke!
Kuna yule jamaa mshauli wa ufundi wa bwana malinzi ana jina la asili ya mkoa wa kagera naomba mwenye CV yake juu ya uweledi wake kwenye mambo ya soka hadi kupewa nafasi hiyo nyeti ya kumshauli Rais wa TFF mambo ya ufundi?serious kuna mambo yanaendelea kwenye soka letu mmmmh yangu macho na masikio.
Timu itacheza Dar es salaam na Zimbabwe mh Rais kuna umuhimu gani wa kuweka kambi mbeya sehemu yenye baridi na viwanja vibovu vya mazoezi ata mechi.
Sijalisoma,nitalitafuta nilisome.All in all hivi ukitaka umkosoe mtu kuna ulazima gani wa kumtukana? Tatizo yeye mhariri wa nipashe amejaliwa kuwa na kalamu na anajua anaowatukana hawana kalamu ya kumjibu,aendelee tu kunitukana,Mungu ni wa wote.Binafsi ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kuwa i am doing my best for Tanzania football tumefanya programme ya uboreshaji timu ya Taifa imetuzalishia wachezaji watano wapya wa National team na watatu wa under 20,uwanja wa karume na Tanga tunamalizia michoro na pesa za kuanzia mradi tumepata,Nyamagana /kaitaba Engineer wa FIFA anakuja wiki ijayo kwa ajili ya nyasi bandia,tukijaliwa January mwakani tutaanza merchandising ya jezi mpya za timu ya Taifa,national youth development plan tunamalizia kuiandaa,tatizo ni nini hasa mpaka mhariri wa nipashe aamue kunitukana?
Tukuyu umefika ukaona quality ya pitch? Unasemaje "viwanja vibovu"? Kumwondoa Kim tuliangalia long term future ya national team na youth football development na sio mechi moja,mpira unajengwa.
Rais wangu Malinzi,nafikiri hizo ndio changamoto zenyewe za Uongozi...
Hebu ungesoma kwanza hiyo Makala then ujue unaweza ukaona kama kuna matusi au laaah...
Kwa ufupi lakini Watanzania tunataka tuone Matokeo chanya kwenye soka letu....Tumechoka Tumechoka kuwa wasindikizaji wa nchi nyingine kwenye michuoano ya kimataifa....
Hizo National Youth Dvlp Plan tumezisikia sana tokea tawala zilizopita lakini waaaapi..au kuna maslahi huko?? Hao vijana mnaowandaaa miaka yote wapo wapi???
Nendeni hapo Ivory Coast mkajifunze kwenye kituo cha ASEC Muone vitendo na maneno kidogo...
Simamieni sheria kikamilifu hususani kwa klabu zetu ziwe za kisasa ili tupate wachezaji wazuri....
Tunekwama,tumekwama na Hatuoni kama mna dalili za kutukwamua...
Ndugu rubaman agandi gandi?Anyway, naona hutaki kujibu maswali ya Malafyale kwa sababu zisizojulikana
Hoja zako hapo juu majibu ninayo nitakujibu.Believe me we are on a right path.
Ndugu rubaman agandi gandi?
Mkuu wala haina haja ya kumuambia chochote Jamal Malinzi kwani ipo confirmed kuwa huyu Mlangira mwenzako ni mbambaishaji tu;Katurudisha enzi za utawala wa hovyo hovyo wa Ndolanga na Rage!
Wkt tuna mechi ngumu na Zimbabwe within a weeks lkn jana anatuambia tujiandae kupiga kura kuchagua jina jipya la kuipa Taifa Stars!Huyu mtu sielewi hata alimshinda vipi Nyamlani
Unamfukuza kocha Kim mapema lkn unamleta mbadala wake weeks 2 kabla ya mechi ngumu na Zimbabwe na akirithi chaguo la wacgezaji toka kwa incompetent Mayanga na Madadi!Miaka 4 mingine ya maumivu kwenye soka letu
Mechi inachezwa Dar kwenye joto lkn unaipeleka team Tukuyu kwenye baridi kali hadi usiku inadondoka barafu!Wakili Mtingojela alikuwa sahihi kukata jina la Malinzi kwa mustakabali wa TZ!Maneno aliyoniambia Rukambura sasa yananiingia akilini!
Tutegemee makubwa zaidi ya haya mkuu maana hii sera yake mpya Jamal Malinzi sijui team ya maboreshe HAIJAWAHI KUWEPO sehemu yyt duniani zaidi ya TZ
Mpira ni sera za muda mrefu sio kama hizi za TFF!Hawa vijana wa Tukuyu kabla hawajaenda Tukuyu walikuwa wapi?Walifundishwa na nani?Maneno ya kaka yangu Rukambura kuhusu mategemeo mengi ya watz kuhusu Malinzi naanza kuyakumbuka sasa!
Malinzi ni mbabaishaji tu kamaure you akina Rage enzi zile
Huyu Mainzi bora ya Ndolanga!
Hakuna kitu hapo, ni ujinga tu!
Kaka Jamal; hoja yangu kwako kwa sasa ni ndogo sana.
timu ya Taifa isiwe mahali pa kukuzia vipaji.
Kila timu ya Premier League (ya Tanzania) si inayo timu ya vijana?
Tena bado kuna timu za vijana za Taifa?
Timu ya taifa inafaa iwe ni mkusanyiko wa wachezaji waliofanya vizuri kutoka katika timu zao.
Kujaza machipukizi taifa kutachelewesha sana mafanikio.🙂
Mheshimiwa rais Tukuyu nimefika nimekaa Rungwe kwa project fulani miezi miwili naufahamu huo uwanja wa chuo ni kwamba ubora wa nyasi zake hauwezi kuwa sawa na uwanja wa taifa ambapo mechi itachezwa lakini mheshimiwa mbona hujajibu issue ya weather sababu kiukweli mbeya hiki ndio kipindi cha baridi kali.
Kitu kikubwa nakuomba sana ndugu Rais usipachoke hapa kuwa mvumilivu jibu hoja kama unavyofanya usiwe na jazba naamini wote tuna lengo moja la kujenga soka letu nauona mchango wa jukwaa hili utapata mengi hadi yale ya uvunguni kuliko watu waongelee chumba acha waongee hapa na wasio wastaarabu watukune lakini usichoke kuwajibu wote mwisho wa siku utapata matokeo chanya kwenye mipango yako TUKO PAMOJA.