Maswali kumi kwa Prof. Kabudi

Kiukweli, bado raisi wa Zanzibar ana chaguliwa Dodoma hilo hata ubishe vipi but ndio jibu lake; unakumbuka uchaguzi wa mwaka 2000, ccm Zanzibar iliwaweka kina Dr. Bilali kwenye top 5 candidates ili kupeperusha bendera ya rais wa Zanzibar na Karume Jr wala hakufikiriwa kabisa, all the sudden Karume Jr ndiye aliyekuja kua mgombea na hatimae kua rais wa Zanzibar na Dr. Bilali akawa mgombea mwenza wa muungano, hapo bara tayari ilichagua (for this case Mkapa ndiye aliye mchagua). Uchaguzi wa 2010 again, nyie huko kweny Zanzibar mliisha apa kwa miungu yenu kwamba hakuna Mpemba atakae kua rais wa visiwa hivyo, kama kawaida ccm Zanzibar ilikua na majina yake, Dodoma kama kawaida ilimchagua Mpemba Dr. Shein kua mgombea uraisi Zanzibar (in this case Kikwete ndiye aliyempa uraisi Dr. Shein).
Mkiwa kwenye bunge lenu huko Zanzibar wabunge wote kwa pamoja hua mnausema vibaya muungano but wabunge wa ccm wakifika Dodoma tu akili zote huahamia Kidodoma Dodoma, bado nina amini hata Jecha alishinikizwa na BARA kufanya alicho kifanya, nina amini hivyo and this si why wakati team ya mpira wa miguu Zanzibar ilipofanya vizuri kwenye mashindano ya CECAFA the former president Kikwete ali tweet kuipongeza, JUSA kwa kujua mambo fulani alimlaumu sana Kikwete kwa matokeo ya uchaguzi mkuu ulio pita hadi Zitto aliingilia kati. Bado nina amini Zanzibar sio nchi, labda jibu la mwisho, passport yako ya kwenda nje ya nchi inatengenezewa Dar au Zanzibar!?
 
Kasome vixur katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndo utaona nafasi ya Rais ya Zanzibar katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Ninachokumbuka kipindi cha uchaguzi, wakati watu wanasema Maalim Seif kashinda na wengine wanasema Shein kashinda, ilileta mtafaruku hadi watu kumtaka rais wa muungano aingilie maswala hayo lakini hakuingilia mambo ya Zanzibar kwa vile hakuwa na mamlaka, duh! Sahivi ana mamlaka, Kwa mantiki hiyo kipindi kile kulikuwa hakuna kifungu kinachompa mamlaka ya kikatiba lakini sahivi kipo?[emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Mabishano ya nini ? Ni wazi kabisa katika katiba Zanzibar ni sehemu ya jmt hivyo sio nchi kamili,ni sehemu tu ya nchi-tanzania
 
Sehemu nyingine ya muungano ni ipi?
 
Jamani wajuzi was lugha ya malikia nisaidieni kutafsiri "Zanzibar is a semiautonomous state" within a complicated and controversial union!
Last not least (i)is Zanzibar a state or nation within a union?
(ii)has Zanzibar ever ruled itself before colonialism and post colonialism?
(iii)can Zanzibar stand on her legs outside the union?if yes,how would Zanzibar tackle the threat of terrorism that is gaining momentum in the East Africa coastline?
If no why?
Mwisho naomba mtoa mada amtumie Profesa Kabudi ayo maswali ili tupate majibu.
 
ati alikuwepo kwenye tume ya katiba ikaja na mapendekezo ya muungano wa sirikali tatu!imenikumbusha yule aliyelikana andiko lake la Phd
siyo huyo wa phd tu,mwingine naye alishadidia serikali3 lkn alipopewa ulaji akawa kama kazaliwa upya hajui kama alikuwa kwenye tume ya warioba,
 
Prof.PARAMAGAMBA J.M.KABUDI hakuna alichokosea bali ameelezea uhalisia ulioko kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Tulielewe hilo kabla ya kumshambulia kwa maneno maana yeye hajaitunga katiba hiyo ya 1977.
 
Umemaliza!
 
siyo huyo wa phd tu,mwingine naye alishadidia serikali3 lkn alipopewa ulaji akawa kama kazaliwa upya hajui kama alikuwa kwenye tume ya warioba,
haya majitu ndio yanampa kichwa Donald azidi kututukana
 
Profesa Kabudi yupo sahihi kabisa, tatizo tulilonalo sie ni kumjadili mtu badala ya kuijadili katiba. Tubadilike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…