Masikitiko makubwa kwa vijana wa zamani

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
1092434

Tumepoteza mwanamziki mwibgine aliekuwa nguli enzi zake, Beresa Kakere, aliyeimba nyimbo kama
  1. Asiya (na Bima) - Asiya eeh Asiyaa, Asiyaaa, Asiyaa mwanakwetu mama Asiyaa, kitendo ulofanya si cha busara
  2. Remmy (na Bima) - Mtoto muaminifu, mtoto mwenye heshima, mtoto mwenye huruuuma Remmy sintakuacha
  3. Magret (na Dar International) Magret mama, shangazi yako anakuita ooh...Kulala kwako mjini faida zake umeziona, wazazi wako wawili sasa wameshakutoka
  4. Sogea Karibu (na Juwata Jazz) Nilikupeleka kwa wakwe zako, ukaonane na ndugu zangu eeh, hata mama yangu alifurahi sana...Sasa nasikia, umefanya visa vingi, hata mama yangu, humthamini
  5. Utu ni Tabia Njema (na Juwata) - Nasikikitika kijana wee, ubadili mawazo yako nakuonea huruma. Umempata wako, wa kukuweka ndani, fani zote za ndani anakutimizia....
  6. ....na vingine vingi.
Kwa wale ambao tulikuwa enzi za miziki hii inasikitisha sana tunapowapoteza hawa manguli, tukiwakumbuka kina Mbaraka Mwishehe, Marijani Rajabu, Hemed Manet, Muhidin Gurumo, Nico Zengekala, Eddy Sheggy (Nikitazama milima ya kwetu eeh, machozi yanitoka kwa uchungu wa mawazo, Shakaza, nk)

Tuambizane wanamziki wengine waliotutoka na nyimbo zao tunazozikumbuka. Siwasahau ni Kasaloo Kyaka na Kyanga Songa, wana Kinye Kinye Kisonzo Fimbo Lugoda Mangala Dance, hasa na kibao chao cha Masafa Marefu (Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu, najua hapa unabaki watasema mengi) au Mapenzi Pesa (Siku hizi mamaa, mapenzi pesa mbeele, yashangaza, utawakuta mtu na mke wake, wakitembea, kama baba na mwana)

Hizo zilikuwa enzi za mziki wenye mashauri haswaa. Sasa siku hizi tunachosikia ni upuuzi wa nikatie, siju niteleze nk. Matusi ovyo ovyo. Ujinga mtupu,
 

Attachments

  • 1557387604773.png
    1557387604773.png
    20.5 KB · Views: 20
Back
Top Bottom