Masikini mimi kijana mwenzenu, nimekua chambio(toilet paper)

Negotiator

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
303
225
Niliponunuliwa dukani nilijua napelekwa kwenye nyumba ya kifahari na kuondokaa dukani palipojaa vumbi na harufu ya panya wakijitafutia riziki. Nilifarijika na kushangilia nafsini mwangu kuona nahifadhiwa kwenye kabati ya nakshi nzuri. Salaaaleeee nilijua nimeula. Ndipo nilipogundua matumizi yangu kwao, waliponisogeza karibu na kinywa chao nilifikiri wananibusu, la hasha! walinitemea makohozi, mate na kunifutia kamasi, mmmmh unyama huuu, kisha walinitelekeza kwenye ndoo la taka. Dhihaka gani hii??? kama haitoshi waliniweka chooni na kunining'iniza kando, kulikoni kushibishwa harufu ya kinyesi na mikojo ya choo kile!! ndipo nilipogundua kua kazi yangu na manufaa yangu kwao ni kuchambia. looohhh kuwaweka wao safi na maridadi huku mimi nikichafuka na kuyabeba manuko yale. kisha kunitupa nioze pamoja na kinyesi kile na kuteketezwa kwenye choo kile nioze
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom