MASHUJAA watakaobaki katika historia kizazi cha sasa

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,353
21,451
1. John Pombe Magufuli baada ya kuapishwa tu amekula sahani moja na vipele na matambazi.

2. Ibrahim Lipumba amepata misukosuko mingi mpaka amevunjwa mkono na kulala mahabusu akiipigania CUF.

3. Dr Ulimboka, bwana huyu alifikia hatua ya kutekwa kung'olewa meno na kucha.

4. Ndimara alikatwa mapanga akiandika habari za kupambana na mafisadi

5. Daudi Mwangosi aliuawa akiwa katika uwanja kutekeleza majukumu yake

6. Dr. Slaa alipigwa mabomu Arusha akaingia chini ya spika kujificha kipindi hicho akiipigania CHADEMA ya kweli.

7. Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu ambaye alituletea serikali ya wala rushwa na mafisadi halafu akawalinda kuliko marais wote.

8. Joseph Sinde Warioba yeye ndie aliosimamia rasimu ya mabadiliko ya katiba mpya

9. Freeman Aikael Mbowe yeye miaka yote alipigania miaka kuhakikisha CHADEMA inapata mgombea makini wa urais

10. Mzee Kingunge baada ya kuangaika na chama kuona kinaishiwa pumzi ikabidi abwage manyanga.

Orodha hii bado ni mbegu unaweza kuongeza unayeona nimemsahau.
 
11. Chenge wa Ufisadi wa Escrow na Rada kuingia kuongoza Bunge Chini ya Serikali inayojitapa kukomesha Rushwa na Ufisadi.
hapa ndipo huwa naona akili za watanzania zimeganda,chenge alipokuwa mwanasheria Mkuu wa seriakali amefanya ufisadi wa kutosha na leo watu wapo humu wanamsifia magufuli kwa nini asimtumbue chenge
 
hapa ndipo huwa naona akili za watanzania zimeganda,chenge alipokuwa mwanasheria Mkuu wa seriakali amefanya ufisadi wa kutosha na leo watu wapo humu wanamsifia magufuli kwa nini asimtumbue chenge
Nionavyo Mimi Magufuli hana uwezo wa kuwashughulikia Mafisadi Papa ambao ni Wanachama wa CCM kwa hofu ya kuuokosa Uenyekiti na kuhofia kunyimwa kura za maoni katika kugombea tena awamu wa Pili.

Chukulia mfano Ufisadi wa Lugumi, Escrow, Meli Chakavu, Nyumba za Serikali, Richmond/ Dowans, Kagoda, Meremeta, Rada n.k. Yote hayo yamefumbiwa macho. Tena alisikika akisema eti tusifukue makaburi, kama alimaanisha makaburi haya ya Ufisadi, basi hatufai.
 
Inaonekana Magufuli kawauzi sana,, wapinzani. Wambieni wabunge wapige kura ya kutokua na imani nayee sasa.

Manake kuna kubwabwaja kwingi sana juu ya utendaji wake. Yani mnavokazania kushindwa kwake utafikiri yeye ni Mungu, sasa nyie mko bize na kuwaza udhaifu wake.

Kwa jinsi mnavomvunja moyo hivi mnafikiri lowasa yeye angefanya nini zaidi ya haya.?? Badala ya kutoa maoni ili kurekebisha hayo madhaifu ili tusonge mbele
 
Snurah. Huyu ni shujaa wa mashujaa. Atabak katika vitab na kumbukumbu ya watanzania wote vizaz na vizaz had milele.
 
MCHUNGAJI MTIKILA....aliipigania Tanzania na ni mtanzania wa kwanza kuishitaki SERIKALI akashinda japo ameshawahi kuwekwa rock up mara 40 na kufungwa mara 3 kwa kesi za kusingiziwa....alishawahi kususia bunge la katiba akajitoa baada ya bunge hilo kukatAa kuwapa WAZANZIBAR nchi yao
 
Nimependa hapo namba saba.Ni sawa na mchungaji aliyefungulia mifugo yake na kuiacha ijitafunie hovyo mazao ya watu bila udhibiti.
 
Peter Tino (Augustino Peter) aliyefunga GOLI lililoipeleka Tanzania katika Fainalii za Mataifa ya Afrika. Hii ni nafasi pekee ambayo Inji hii imepata kupata katika mashindano hayo.....
 
Back
Top Bottom