Mashine za TRA Watanzania hawazielewi! Hata uwaandikie 500 kitu cha 500,000 hawaelewi

kaseva

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
473
305
Watanzania wameanza kudai sana risiti baada ya wito wa Rais n.k
but
Raha mustarehe kwa wafanya biashara wamelazimishwa kuwa na mashineeee
Wamekuwa nazo baadhi yao lakini
Sasa kimbembe kwa watanzania
Hawazielewii
Haata
Kwanza zimeandikwa kimombo
Kama mjuavyo kimombo ni shida toka huko juu
Pili kimeandikwa mambo kibao
Vinachosha kusoma.
Ni advantage kwa wafanya biashara
Ni hasara kwa serikali waandae mbinu nyingine ya kufundisha watu kimombo kwanza.
 
Umelonga point mkuu,

Unalipia mzigo wa laki mbili unapewa risiti ya elfu 70, eti ya kusafirishia mzigo

Aisee kazi ipo
 
Hahaha mkuu nimecheka sana!pale uliposema kimombo ni shida hata huko juu!!!!!kwikwikwi

Ova
 
kuna siku nilienda club nexdoor.. nikapewa risiti ya tra imeandikwa 00 tupu.. sikuone hela niliyolipa na hata sikuelewa.. nikamuuliza akasema ndio zilivyo...
 
Akikuona boya wala hakwambii anakutolea risit kwenye mashine tu, umelipa laki mbili mashine inatoa risit ya elfu 70. KAma akikuona mjanja anakwambia kabisa, hii ni ya kusafirishia mzigo, mpemba mmpja alinambia hivyo kidogo nimpe kibano lakini kwakuwa namjua nikamuacha tu.
 
Ni kweli kuwa utekelezaji wa mradi mkubwa kama huu wa EFD unahitaji elimu ya kutosha kwa wateja na watoa huduma. Ili mashine hizi ziweze kuchangia uboreshaji wa kodi kupitia uzibaji wa mianya ya kukwepa kodi, usahihi wa taarifa zinazoingizwa kwenye mashine ni muhimu sana. Vinginevyo mteja atachukua tu risiti kutimiza majukumu. Kampeni mpya inahitajika, na isilenge tu kwenye 'dai risiti', iende mbele zaidi na kusema 'dai risiti sahihi', au 'soma risiti'
 
Back
Top Bottom