Mashine za kutengeneza mkaa wa kisasa za manual yaani unatumia mkono zinapatikana. Bei inatofautiana kutokana na size ya mashine. Ila ndogo kabisa inaanzia sh. 50,000 inayoweza zalisha gunia kuanzia mbili mpaka tatu zile kubwa kabisa. Mashine kubwa kabisa ni ya sh. 100,000 inauwezo wa kuzalisha gunia kuanzia 4 mpaka 5.
Ukinunua mashine hizi pia tunakufundisha jinsi ya kuibadilisha na kuwa ya umeme na kuongeza uzalishaji hadi kufikia gunia 15 kwa siku. Kama utaona kununua mashine ambayo iko tayari ni pesa nyingi, unaweza tengeneza yako mwenyewe. Kuanzia wiki iliyopita kitabu ninachokiuza cha jinsi ya kutengeneza mkaa wa kisasa kimeongezwa kurasa zinazoonyesha jinsi ya kutengeneza mashine yako mwenyewe. Hii itafanya upunguze gharama kwa kiasi flani.
Imenilazimu kuingia youtube kujionea kazi hii na maishine hii.....Nimejifunza kitu ikiwa ni pamoja na kusambaa kwa ujuzi huu nchi mbalimbali ikiwemo kenya.....pia nimeshawishika na uzalishaji wa bidhaa hii kama kiwanda kidogo.....Nikijaaliwa sitalazia damu ila nitahitaji uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kutembelea kiwanda chochote husika.....kama morogoro kipo naweza kuelekezwa nikajionea na kujifunza zaid....Nafurahi namna watu wanashirikishana ktk fursa kama hivi...Nikupongeze mana umenitoa tongotongo ijapo nilishapata kuuona huo mkaa ila sikuutilia maanani....Niahid kuendelea kujifunza zaidi nikiendelea kujichanga.