...Zikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa mashindano ya kombe la Afrika,masikio na akili za watanzania zimetegemee kusikia uchambuzi wa kijinga na kinazi toka kwa hawa wachambuzi wa kitanzania ndugu Edo Kumwembe na Shaffiii Dauda...Jamaa wana uchambuzi wa kinazi,usije ukashangaa wanatabiri ubingwa kwa zile timu zenye wachezaji wa timu zao wanazoshangilia kule Ulaya...Niliwai kumsikia Edo akisema kuwa wao uchambuzi wao ni mpana,wanasikiliza kauli za makocha wa ulaya na kuzitolea ufafanuzi na sio kuzitangaza kama zilivyo,hap alikuwa anaongelea kile kipindi chao cha Sport Extra....
....Ki ukweli jamaa wako very shallow na si wachambuzi bali ni washabiki wa mpira wa miguu na ndio maana nasema tegemeeni uchambuzi wa kijinga na kitoto toka kwa Edo Kumwembe na Shaffii Dauda very soon.
Pole mkuu, ila bado mna mechi za kujirekebisha.. Chipolopolo hoyeeeeeeeeee!!!Kama kawaida yetu, vipi wenzangu mshachagua timu (Nchi) za kuzishabikia/kuzishangilia? Mimi nitakuwa nawashabikia/nawashangilia Senegal. Pale kuna wachezaji wawili wa timu ninayoishabikia England (Newcastle United): Demba Ba (wapenzi wa Man U wanamtambua huyu) na pia yupo Demba Cisse (huyu msiomfahamu, mtaziona cheche zake hapo AFCON na baadaye kwenye EPL).
Kila la Heri!
Je hao akina edo watakuwa wanachambua recorded match! (au watakodiwa na dstv) maana sujaona kama kuna local channel itakayoonyesha live.
Mtoa mada nakuomba utoe hapa jukwaani uchambuzi makini kuhusu mechi hizo, maana wewe inaonekana hauna uchambuzi wa kijinga na kitoto. Kweli miafrika ndio tulivyo, wewe baada ya kuona uchambuzi wao haufai ulichukua hatua gani?
Je, uliwapa japo hata ushauri.?