Mashindano ya afrika hayo...tegemea uchambuzi wa kijinga toka kwa edo kumwembe na shaffii dauda..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashindano ya afrika hayo...tegemea uchambuzi wa kijinga toka kwa edo kumwembe na shaffii dauda.....

Discussion in 'Sports' started by only83, Jan 19, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...Zikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa mashindano ya kombe la Afrika,masikio na akili za watanzania zimetegemee kusikia uchambuzi wa kijinga na kinazi toka kwa hawa wachambuzi wa kitanzania ndugu Edo Kumwembe na Shaffiii Dauda...Jamaa wana uchambuzi wa kinazi,usije ukashangaa wanatabiri ubingwa kwa zile timu zenye wachezaji wa timu zao wanazoshangilia kule Ulaya...Niliwai kumsikia Edo akisema kuwa wao uchambuzi wao ni mpana,wanasikiliza kauli za makocha wa ulaya na kuzitolea ufafanuzi na sio kuzitangaza kama zilivyo,hap alikuwa anaongelea kile kipindi chao cha Sport Extra....

  ....Ki ukweli jamaa wako very shallow na si wachambuzi bali ni washabiki wa mpira wa miguu na ndio maana nasema tegemeeni uchambuzi wa kijinga na kitoto toka kwa Edo Kumwembe na Shaffii Dauda very soon.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duh kwa hiyo bora hata dr leakey nini kuliko kina shaffih ngoja tuone..
   
 3. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mmmh...., hata kama namchukia mtu, siwezi kumsema vibaya hivi bali ningemshauri ajirekebishe kwenye maeneo yenye mapungufu.
   
 4. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Kama kawaida yetu, vipi wenzangu mshachagua timu (Nchi) za kuzishabikia/kuzishangilia? Mimi nitakuwa nawashabikia/nawashangilia Senegal. Pale kuna wachezaji wawili wa timu ninayoishabikia England (Newcastle United): Demba Ba (wapenzi wa Man U wanamtambua huyu) na pia yupo Demba Cisse (huyu msiomfahamu, mtaziona cheche zake hapo AFCON na baadaye kwenye EPL).
  Kila la Heri!
   
 5. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Goma linaanza kesho hilo! Magwiji wote wa afrika nje.
   
 6. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  edo nafuu lakini shafii ni bora mbwiga wa mbwiguke
   
 7. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Je hao akina edo watakuwa wanachambua recorded match! (au watakodiwa na dstv) maana sujaona kama kuna local channel itakayoonyesha live.
   
 8. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Walete unazi ila senegal fainali inatuhusu!!!!
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, ila bado mna mechi za kujirekebisha.. Chipolopolo hoyeeeeeeeeee!!!
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwenye spoti xtra na spoti baR
   
 11. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada nakuomba utoe hapa jukwaani uchambuzi makini kuhusu mechi hizo, maana wewe inaonekana hauna uchambuzi wa kijinga na kitoto. Kweli miafrika ndio tulivyo, wewe baada ya kuona uchambuzi wao haufai ulichukua hatua gani?
  Je, uliwapa japo hata ushauri.?
   
 12. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Na akishakumaliza kuchukua hatua na kuwapa ushauri hao anaosema 'wanazi' badala ya kuwa wachambuzi, tunamtaka atuanzishie Thread(uzi) hapa JF ya uchambuzi makini wa mashidano hayo yanayoendelea ya kombe la Afrika
   
 13. T

  TUMY JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umekurupuka kusema Edo kumwembe na Shaffih Dauda wana uchambuzi wa kijinga,na inaelekea wewe mpira huufahamu umeanza ushabiki ukubwani suala la kuuchambua mpira halina maana kwamba ndivyo itakavyokuwa kwa asilimia 100, nenda kwenye website ya BBC Sport utajifunza mambo mengi wanachambua na bado wanakosena sana tu ila ni uchambuzi kwa jinsi wanavyoona wao kwa kipindi hicho kwa hiyo uchambuzi unaegemea kwenye vigezo fulani vya mchambuzi haina maana kwamba wako pale kukuambia leo huyu lazima afungwe hapana.Acha kukurupuka kulaumu watu wakati thana nzima ya uchambuzi inaelekea huifahamu. Wabongo mnajua kukosoa tu, nenda kauchambue wewe tukuoneukifikiri ni kazi rahisi.Watu wengine bwana.
   
Loading...