Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Katika jitihada za kupambana na uingizaji na utumiaji madawa ya kulevya kisiwani Zanzibar baadhi ya masheha wamelilalamikia jeshi la polisi visiwani hapa kwa kile walichokiita ushiriki mdogo kwenye mapambano dhidi ya janga hilo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina masheha(viongozi wa mitaa) hao walisema licha ya kuundwa kwa kamati maalumu za wazee kwenye shehia zao kwa lengo la kukabiliana na vitendo viovu kwenye jamii bado wamekua wakikumbana na changamoto mbali mbali.
Walisema kuwa kwa sasa visiwani hapa kumekuwepo na ukithiri mkubwa wa utumiaji na uingiaji wa madawa ya kelevya lakini jambo la kushangaza hadi sasa polisi wameshindwa kutoa ushirikiano wao kikamilifu.
Walieleza kuwa wakati wengine wanafikia mpaka kutoa taarifa za watumizi wa madawa hayo na vigenge vyao lakini chakushangaza hawaoni hatua yoyote hile inayochukuliwa na jeshi hilo ikiwemo kuwakamata wahusika.
‘’Kwa mfano ndugu mwandishi hapa katika shehia yangu wapo baadhi ya askari ni watumiaji wa madawa ya kelevya (bangi )na ndio maana wanashindwa kutoa ushirikiano tunapopeleka taarifa zetu’’alisema mmoja miongoni mwa masheha hao.
Akitolea ufafanuzi juu ya tuhuma hizo kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame alisema inawezekana wapo baadhi ya watendaji kwenye jeshi hilo wanaotumia madawa.
Alisema wao kama jeshi la Polisi wamekua na utaratibu maalumu wa kuunda vikosi kazi vya kupambana na hali hio kwa lengo la kuonesha ni jinsi gani serikali inaathiriwa na matumizi ya madawa kwa vijana wake.
Makame aliitaka jamii kutoa ushirikiano na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa juu ya watumiaji na waingizwaji wa madawa ya kulevya au iwapo watakuwa na taarifa yoyote hile mbaya.
Kamishna huyo aliwatoa wasiwasi wananchi na kuwataka wasikate tama kutoa taarifa na iwapo wanahisi taarifa zao hazikufanyiwa kazi wafike ngazi za juu zaidi.
‘’Hata mimi mwenyewe naumizwa na jambo hili la utumiaji wa madawa ya kelevya na iwapo itatokea mtu hata akiwa na taarifa mbaya dhidi yangu basi na akatoe taarifa kwa mkuu wa jeshi la polisi ‘’ alifafanua zaidi kamishna huyo.
Pamoja na hayo Hamdan alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuishi kwa dhana badala yake wawe mstari wa mbele kutoa mashirikiano na jeshi hilo kila wakati kwa lengo la kujenga jamii iliobora hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Chanzo: Habari Kwanza