Hawa Asec wa sasa hawana mpira wowote Simba akifungwa na hawa utakua ni uzembe mkubwa sana. Wanafungwa fungwa tu huko ligi ya kwao. Kwakifupi kwenye kundi la Simba akikaza anaongoza hilo kundi kuelekea robo fainali. Pamoja na ubovu wa Simba kwa sasa na kukosa kocha lakini sioni timu ya kuisumbua Simba kwenye kundi lao. Simba atakwenda robo fainali tena kwa kishindo kikuu
Mimi nafikiri bado Wana simba hawataki kusema ukweli kutokana na kuwa muddy kaitoa mbali na kuifikisha hapo japokuwa ni kwa muendelezo wa miaka 4 hivyo imepanda kiwango ila mimi naweza sema kutokana na juhudi binafsi za wachezaji, sapoti ya wana Simba, morali na hata uongozi wa babra apewe maua yake. Baada ya kuuza wachezaji wakubwa, wazuri na waliokuwa wanajituma matokeo yake kwa Sasa simba ina shida maana huenda baada ya hela kuingia simba basi MUDDY kaamua ajirudishie maana ni juhudi zake binafsi na sio hawa wamiliki wa 51% ambao hawana msaada wala kutoa hela. Mapendekezo yawe hivi.
1. Kufikia malengo, simba iamue kuwa kuanzia Sasa wachezaji wawe wanatoka nje ya nchi jirani hizi za Rwanda,burundi,kenya,uganda tuachane nao na twende huko Nigeria, ghana, Benin, South Africa, nk
2. Timu iweke mapendekezo ya kuanzishwa kwa kadi zenye hadhi maalum kuanzia za million, million mbili hadi hata 5 ili hawa wakitoa hizo hela basi kila mwaka hawatakuwa tena watoe hela za kiingilio bali ni Free pass na wawe wanaruhusiwa kwenda na timu nje ya nchi nk.
3. Watu wengine wawe wanalipia michango ya uanachama kwa njia za kadi ambazo zinaweza kuwa attached na bank kwa ajili ya kuchaji hela zao na kulipa ada zao, na hata tickets kama wako nje ya nchi au kulipia kupitia kadi zao.
4. Pia kwa watu walioko nje ya nchi nao wanaweza pata kadi zao kupitia hata kwa mawakala au utaratibu ufanyike ili wapate kadi na kulipia michango yao.
5. Walau hao wenye hadhi maalum hao watakuwa wanapata bonuses mbali mbali kama kupiga picha na wachezaji, kupata mialiko mbali mbali ya simba, kupewa jezi pindi zikija nk
6. Kujua idadi ya watu wao na michango na hata kuanzishwa kwa kadi hizo zitumike hapo hapo uwanjani ambapo akiweka kadi inaprint anaondoka.
7. Kuwepo na renewable kila mwaka.
8. Pia kuwepo na vitu vingine viwe advertised kama funguo, viatu, nk
9. Awepo afisa biashara ambae atakuwa na wajibu wa kuratibu masuala ya kibiashara kwa kutafuta wadhamini tu ndani na nje ya Tanzania nafikiri hapo tunaweza kuza Brand ya Simba.
10. Kwa kuwa simba inajitangaza pia kupitia jezi yake, Basi afisa biashara awe anatangulizwa kwenye nchi husika and then kuratibu jezi za timu ili iwapo timu inacheza basi wale washabiki wawe na jezi.
Hapo timu inaweza kuza Brand yake,kupanda kwenye chati ya timu ambazo zina hela na pia kusajili wachezaji wa bei mbaya.
Sasa kumwachia muddy kila kitu hapo wanachama wanafeli Sana na kusubiri tu kuchagua viongozi sio vizuri.
Suala la kumuuzia jamaa muddy hisa 49% napo naona kama wangewauzia watu wawili kwa kiasi cha walau billion 25 kwa nusu hisa za MUDDY na yeye atoe billion 25 ingekuwa vizuri Zaidi.
Nasikia kuwa BHAKRESA aliitaka simba ila akachomolewa kisa atakuwa na timu mbili wakati Azam ni timu ya watoto wake.
Tofauti na nilichosema,tutaishia kununua wachezaji wa buku buku,kufungwa Hovyo na muddy kutukanwa na kutaka kuiacha timu. Wachezaji wanaotakiwa Simba ni wengi na wengine wanataka ili kuonyesha makali yao ila inapokuja kwenye hela MUDDY ni mbahili na pia kuna wapigaji Sana. Tuambie kipa asie na kiwango, kocha asie na kiwango, wachezaji wazawa akina chilunda na wenzake wa bei rahisi wako wapi kama sio benchi?
Wachezaji akina okra,akra,yule beki nimesahau jina lake,na Sasa wanawaleta akina adebayor, manzoki ambao ni Free agent na hawachezi mpira kwa muda. Muddy kutoa hela ni shida ngoja ifungwe tu maana hata kumfukuza huyo kocha ni kuficha mambo yao na wachezaji wamesema ishu ni posho zao hawapewi,try again na mangungu nao wanakaa kwenye uongozi kwa sababu gani?kocha angebaki tu. Nasikia hata kocha wanaemtaka anataka hela nyingi kila wakigusa matokeo yake mgunda anarudishwa. Anyway ngoja huyo Barbra arudi tuone