Kuna aina za viumbe zaidi ya milioni hapa
duniani, lakini sio aina zote zinafaa kwa
chakula. viumbe wengine wana sumu kali na
endapo utawala, basi lazima utakufa.
Mungu wa mbinguni ndiye muumbaji wa vitu
vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana, na
katika hili hakutuacha gizani, ili tutumie hekima
zetu za kibinadamu la, alitoa mwongozo sahihi
kuhusu tule nini tuache nini.
Mara baada ya kuwaumba Adamu na Hawa
Mungu aliwaamuru kula matunda. Mwanzo
1:29. Hiki ndicho chakula cha kwanza kabisa
ambacho Mungu alikichagua kwa ajili ya viumbe
wake aliowaumba.
Ukipewa kuchagua kitu kimoja kati ya vingi ni
wazi kuwa utachagua kilicho kizuri na bora
zaidi. Hivyo matunda yalikuwa chakula bora
zaidi na ndiyo maana Mungu aliyachagua kabla
hata ya dhambi kuingia.
Baada ya Adamu na hawa kuasi na kufukuzwa
bustanini ndipo Mungu akawaamuru kula
matunda pamoja na mboga za kondeni, hivyo
wanadamu wakaanza kupika. Mwanzo 3:18.
Maisha yakaendelea hivyo hadi kipindi cha
gharika. Hadi hapo Mungu alikuwa hajaruhusu
watu kutumia nyama kama chakula lakini
inasemekana watu walikuwa wakitumia bila
kujali maagizo ya Mungu, tena wengine walikula
nyama mbichi.
Wakati wa gharika Mungu anamwagiza Nuhu
kuingiza wanyama katika safina, walio safi
waliingia saba saba walio najisi waliingia wawili
wawili, hivyo ni wazi kuwa tofauti kati ya
wanyama safi na wasio safi ilikuwepo hata kabla
ya Mungu kuruhusu nyama itumike kama
chakula. Wanyama safi ndio waliotumika kama
sadaka mfano ng'ombe, kondoo n.k.
Baada ya gharika ambapo kila kitu kilikuwa
kimeharibiwa ndipo Mungu aliporuhusu
wanadamu kutumia nyama kama chakula.
Mwanzo 9:3. Baadaye, baada ya maandishi
kugunduliwa huko misri, Mungu akaamua
kuweka maagizo yake katika maandishi,
maelezo ya kina juu ya wanyama safi na najisi
yanapatikana katika kitabu cha mambo ya
Walawi sura ya 11.