Maridhiano ni muhimu

Maridhiano ni muhimu

Suleiman Mfua

Member
Joined
Feb 27, 2014
Posts
62
Reaction score
64
MARIDHIANO YA KISIASA NI MUHIMU KWA MANUFAA YA TANZANIA YETU.

Na Mfua Suleimana (Mshamba)


Katika kipindi cha Miaka minne iliyopita nchi yetu imepitia katika kipindi kigumu kisiasa hasa kwa wanachama wa vyama vya upinzani, ugumu huo unatokana na katazo la mikusanyiko ya hadhara ya kisiasa lililotolewa na Mhe. Rais Dkt. John P. Magufuli.

Mbali na katazo la Mikusanyiko ya hadhara iliyopigwa marufuku lakini pia tumeshuhudia mikusanyiko ya ndani kwa baadhi ya vyama vya siasa vya mlengo wa kushoto (Upinzani) nayo ikipigwa marufuku kwa kile kilichoelezwa na taarifa za kiintelejensia kua uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.

Mbali na hayo! Imeelezwa kuwa katika kipindi hicho cha miaka minne, kumekuwepo na Uminywaji wa Demokrasia, uhuru wa kujieleza, ukiukwaji wa haki za binadamu n.k.

Na hayo yamedhihirishwa na baadhi ya vyama hivyo katika mikutano yao na vyombo vya habari walioifanya kwa nyakati tofauti hapa nchini.

Nirudi katika msingi wa hoja yangu. Tarehe 9 December ya kila mwaka ni siku maalum kwa nchi yetu. Kwa kuwa ni kumbukizi ya siku tuliyopata uhuru. Na mwaka huu sherehe hizo zimefanyika katika jiji la Miamba (Rock City) Mwanza.

Moja ya matukio makubwa na yenye kusisimua ni Kambi rasmi bungeni ikiongozwa na Mhe.Freeman Mbowe kushiriki sherehe hizo, hilo ni jambo zuri na lafaa kuungwa mkono na kila mwenye nia njema na taifa letu.

Pia kwa upande mwengine nimpongeze Rais Dkt. John Magufuli kwa kutambua umuhimu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na kuialika kambi hiyo katika matukio muhimu ya kitaifa.

Na jambo hilo lisikomee katika 9 December pekee bali liendelee katika matukio mengine muhimu ikiwemo, ziara za mhe. Rais, uapishwaji wa viongozi n.k.

Kwani kwa kufanya hivyo kutawapa fursa na Watanzania wengine waliochagua kambi hiyo kushiriki matukio hayo kupitia wawakilishi wao.

Lakini pia ni muhimu sana kuzingatia mambo ya msingi yaliyozungumzwa na Mhe. Mbowe (KUB) alipopewa fursa ya kusalimia na Mhe Rais katika maadhimisho ya 9 December pale Kirumba, MARIDHIANO, MARIDHIANO, MARIDHIANO.

Naam MARIDHIANO ni muhimu sana katika taifa letu na hasa kwa wanaofahamu machungu ya Donda la Kisiasa na madhara ya Donda hilo endapo wataacha unafiki.

"NAKUNYWA MAJI KWANZA"

Mfua suleiman(Mshamba)
Mvomero-Morogoro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom