Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 726
- 953
Kuna mkanganyiko mkubwa unaoenezwa kwa makusudi katika mjadala wa kisiasa nchini Tanzania kuhusu dhana ya maridhiano. Neno hili linatumika kana kwamba ni suluhisho la kila tatizo la kitaifa, bila kuzingatia misingi ya kisiasa, kisheria, na kimaadili inayopaswa kulitangulia.
Kwa mtazamo wa kisiasa, maridhiano huwezekana pale ambapo kuna mgogoro wa pande mbili tofauti za kisera, kimtazamo au kimkakati ambapo kila upande una hoja halali zinazohitaji kusawazishwa kwa mazungumzo ya wazi na ya heshima. Lakini maridhiano hayawezi kutumika kufunika au kusafisha uhalifu wa upande mmoja dhidi ya wananchi.
Katika muktadha wa sasa, CHADEMA haina mgogoro wa kisiasa na CCM wala na serikali. Kilichopo siyo mvutano wa hoja, bali ni ukiukwaji wa wazi wa sheria na Katiba unaofanywa na dola dhidi ya raia wake. Kwa mifano isiyo na ubishi:
Haya si mambo yanayohitaji maridhiano. Haya yanahitaji uwajibikaji wa kisheria. Pale ambapo kosa linatoka upande mmoja, hakuna mgogoro wa pande mbili wa kutatuliwa kwa maridhiano. Kuna mhanga na kuna mkosaji.
KWA MTAZAMO WA KIMUNGU, MARIDHIANO HAYAWEZI KUTANGULIA HAKI
Kwa mtazamo wa Kimungu (kiroho) maridhiano ya kweli huja baada ya ukweli kusemwa, dhambi kukiriwa, na haki kutendeka. Bila hayo, maridhiano hubaki kuwa ubatili wa kisiasa na udanganyifu wa kimaadili na uovu mbele za Mungu.
Maandiko Matakatifu yanaeleza wazi:
“Haki, haki peke yake, ndiyo utakayofuata.” (Kumbukumbu la Torati 16:20). “Msingi wa kiti cha enzi ni haki na hukumu.”(Zaburi 89:14).
Kwa hiyo, swali la msingi linalopaswa kuulizwa na kila Mtanzania Je, Maridhiano ya aina gani yanazungumzwa?
Maswali haya yote yanatoa jibu la kwamba huo siyo msimamo wa kisiasa unaolinda demokrasia, haki na uwajibikaji wala siyo msimamo wa Kimungu unaothamini utu wa binadamu, haki za watu na amani kwa watu wote.
📌Amani ya kweli haiwezi kujengwa juu ya dhuluma, na utulivu wa juu juu hauwezi kuchukua nafasi ya haki.
Kwa mazingira ya Tanzania, kuhimiza maridhiano bila kuzungumzia haki, sheria, na uwajibikaji ni kuhalalisha uonevu kwa lugha laini. Ni kugeuza siasa kuwa chombo cha kuficha uhalifu, na dini kuwa kifuniko cha ukimya.
Nimalizie kwa kusema hivi maridhiano bila haki siyo suluhisho ni ubatili, ubatili mtupu. Taifa linahitaji haki itendeke, sheria ziheshimiwe, na wote waliokabidhiwa mamlaka wawajibike. Hapo ndipo maridhiano ya kweli, ya kisiasa na ya kimungu, yanaweza kuzaliwa.
📌Maridhiano bila haki ni dhambi. Amani bila ukweli ni uongo. Utulivu unaojengwa juu ya damu ya wasio na hatia ni laana, si baraka.Kinachohitajika Tanzania si maridhiano ya kisiasa, bali ukombozi wa haki"
ASKOFU MWANAMAPINDUZI
28.01.2026

- Wizi wa kura ni kosa la jinai
- Utekaji na kupotezwa kwa watu ni uhalifu mkubwa
- Kubambikizia wananchi kesi ni matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Kunyima haki za kikatiba si tofauti ya kisiasa, bali ni uvunjaji wa Katiba.
- Ufisadi ni kosa la jinai na uhujumu wa uchumi wa taifa
Haya si mambo yanayohitaji maridhiano. Haya yanahitaji uwajibikaji wa kisheria. Pale ambapo kosa linatoka upande mmoja, hakuna mgogoro wa pande mbili wa kutatuliwa kwa maridhiano. Kuna mhanga na kuna mkosaji.
KWA MTAZAMO WA KIMUNGU, MARIDHIANO HAYAWEZI KUTANGULIA HAKI
Kwa mtazamo wa Kimungu (kiroho) maridhiano ya kweli huja baada ya ukweli kusemwa, dhambi kukiriwa, na haki kutendeka. Bila hayo, maridhiano hubaki kuwa ubatili wa kisiasa na udanganyifu wa kimaadili na uovu mbele za Mungu.
Maandiko Matakatifu yanaeleza wazi:
“Haki, haki peke yake, ndiyo utakayofuata.” (Kumbukumbu la Torati 16:20). “Msingi wa kiti cha enzi ni haki na hukumu.”(Zaburi 89:14).
Kwa hiyo, swali la msingi linalopaswa kuulizwa na kila Mtanzania Je, Maridhiano ya aina gani yanazungumzwa?
- Je, ni maridhiano ya kukubaliana kura ziibiwe kwa kiwango kinachoruhusiwa?
- Maridhiano ya kukubaliana Haki za watanganyika ziendelee kukandamizwa na kwa kiasi/kiwango kinachovumilika?
- Maridhiano juu ya maisha ya watanganyika yahatarishwe kwa jina la “amani”?