marekani yapeleka meli za kivita katika rasi ya korea

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,401
8,113
Jeshi la Marekani limetoa amri kwa meli zake za kivita zinazobeba silaha zielekee karibu na rasi ya Korea, huku kukiwa na hofu kubwa kuhusiana na Korea Kaskazini kuimarisha silaha zake za kinukilia.
Msimamizi wa kijeshi wa Marekani wa eneo la Pacific alieleza kuwa kujiandaa huko kijeshi ni muhimu katika eneo hilo.
Meli hizo zinazojulikana kwa pamoja kama The Carl Vinson Strike Group zinashirikisha meli moja kubwa ya kubeba ndege za kivita na meli zingine za kivita za kawaida.
View attachment 493168

Awali ndege hizo zilitarajiwa kuzuru Australia lakini mkondo wake ukabadiliwa kuelekea Bahari ya Pacific.
Eneo hilo la Pacific ni kule ambako wanajeshi wa Marekani walifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.
Msemaji wa jeshi la Marekani anasema kuwa Korea Kaskazini ndilo tisho kubwa zaidi kwa usalama wa eneo la Pacific.

View attachment 493169
Anasema ushahidi ni jinsi taifa hilo linavyofanya mazoezi ya zana za kinukilia kiholela.
Mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia, meli hizo za kivita zina makombora yanayoweza kuzima zana zo zote zinazolengwa kwake.
 
Yan hapo USA wanasubir waguswe tu uone hilo varangati...

Jaribu kuvuta picha iwapo korea itarusha kombora ambalo litagusa au kudondoka karibu na meli za USA, (jus joking)

Isije ikatokea yale ya Vietnam
 
USA anashindwa kushambulia kwa ajili ya south korea na japan ambao watachakazwa vibaya
 
Mpk wahakikishe 100% kuwa jamaa hana nuclear ndio watampiga but also wanajua kuwa China wataingia tu vitani maana North koreas ni decoy country yao kujilinda na wajapan na usa na skorea
 
Hiyo inatafutwa vita ya tatu ya dunia
Marekani hakuwahi kushiriki vita vya dunia vilivyopita.hivyo ana nyenge nayo sana chokochoko zote hizo ili akinukishe.na madhara yatakua makubwa sana kama miaka ile na silaha za kipindi kile kulikua na madhara makubwa sipati picha ulimwengu huu wa nyuklia tutapona kweli.nuclea is to dangerous than atomic
 
Back
Top Bottom