Marekani: Tuko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
947
_95833013_0a21b9d2-32ab-4df4-bb1b-a26c63a906ff.jpg

Image captionRex Tillerson (kulia) na balozi wa Marekani kwenye UN Nikki Haley, wakiwa kwenye mkutano

Marekani iko tayari kwa mazungumzo na Korea Kaskazini yenye lengo la kuondoa zana za nuklia kutoka eneo hilo, kwa mjibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson.

Lakini amesema kuwa Marekani itatumia nguvu za kijeshi ikiwa itahitajika.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa China, mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini, anasema makubaliano ya amani ndio njia pekee.

Bwana Tillerson aliliambia baraza la ulinza la Umoja wa Mataifa kuwa tisho la Korea Kaskazini la kushambulia majirani zake na zana za nuklia.

Maelfu ya wanajeshi wa Marekani wako nchi majirani wa Korea Kaskazini ikiwemo Korea Kusini na Japan.

Tillerson amezitaka nchi wachama wa Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo na kupunguza uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi hiyo.

"Kwa miaka kadha Korea Kaskazini imekuwa ikiendesha kwa nguvu mpango huu hatari."

"Ni wakati wetu kuchukua hatua na kudhibiti hali," Tisho la Korea Kaskazini la kufanya shambulizi la nuklia dhidi ya Korea Kusini au Japan ni la kuwezekana, na ni muda tu kabla ya Korea Kaskazini kufanikiwa kupata uwezo wa kushambulia Marekani." alisema Tillerson.
 
Team Mapanki...

Team Kiduku...

Team Andunje...

Hapa majaribio kwenda mbele tuu, mazungumzo nenda kwa Waarabu kwanza.
 
NO mazungumzo ...Maana mangumzo yoyote yale nikua NK iachane na mpango wake wa Nuclear na Makombora ya Ballistic Kitu ambacho NK hawawezi kukubari....Irak na Libya ni mfano mzuri sana kwa NK....So Kim yeye kashasema Testing of Nuclear and ballistic missiles ipo palepale
 
Hakuna cha mazungumzo hapa aende akazungumze na wala tende ambao alshazoea kuwalaghai mwisho anawatandika haaminiki huyo mbwa mapanki kaza kamba mpaka Trump avue wigi
 
Back
Top Bottom