MAREKANI: Rais Trump anataka Walimu wapewe silaha ili kukabiliana na matukio ya kihalifu shuleni

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,047
Reaction score
3,978
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.

''Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja'', alisema. Bwana Trump alitoa pendekezo hilo huku manusura wa shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Februari wakimtaka kuhakikisha kwamba shambulio kama hilo halitokei tena.

Rais huyo wa Republican pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki. Manusura wengine wakati huohuo waliwataka wa bunge wa Florida kuweka udhibiti wa bunduki.

''Tutakuwa thabiti iwapo kutakuwa na ukaguzi mbali hali ya kiakili ya mtu anayetaka kumiliki bunduki''. Trump aliwaambia wanafunzi kutoka shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas wakati wa hafla hiyo iliorushwa hewani moja kwa moja katika ikulu ya Whitehouse.

''Haitakuwa maneno kama ilivyokuwa awali'', aliongezea. Rais huyo wa Marekani pia aliunga mkono pendekezo lililoungwa mkono na muungano wa wamiliki wa bunduki NRA .

Aliaahidi kuangazia kuhusu wito kwa walimu kupewa bunduki. ''Iwapo una mwalimu ambaye ana bunduki'', alisema ''anaweza kusitisha shambulizi lolote kwa haraka. Iwapo mwalimu angemiliki bunduki , ijapokuwa najua ni swala ambalo lingezua utata, wangepewa mafunzi maalum na wangesaidia pakubwa''.

''Kusingekuwa na uhuru wa kuingia katika shule na kuanza kufyatua risasi, kwa sababu washambuliaji wangekuwa waoga''.

Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.

Rais huyo wa Marekani alisikiliza malalamishi ya mabadiliko ya sheria za umiliki wa bunduki siku ya Jumatano kutoka kwa wanafunzi 40 , walimu na familia.

Baadhi ya wale waliohudhuria hafla hiyo ya saa moja waliunga mkono wazo la rais Trump kuwahami walimu.

Lakini Mark Barden ambaye mwanawe aliuawa katika shambulio la 2012 katika shule ya Sandy Hook Elementary School mjini Connecticut - anasema ''ongezeko la bunduki sio suluhu. Walimu wana majukumu zaidi kwa sasa kwa wao kuchukua jukumu jingine la kutumia nguvu ili kumuua mtu'', alisema.

BBC
 
Nawaza tu hili wazo la walimu kupewa silaha ingekuwa hapa Bongo, na hizi stress zao. Duh
 
Siku mwalimu kichaa kikimpanda ataua wanafunzi wote!! Ni sawa na kuruhusu Pilot awe anasafiri na silaha ila kukabiliana na magaidi..!! Hii sio solution hata kidogo.
 
Trump kashaanza sarakasi. Mamwinyi wa kimarekeni, akinaTrump, wanazipenda bunduki nadhani kuliko wanavyompenda Mungu. Ni ngumu sana kufuta umiliki binafsi wa silaha US kwa sababu mamwinyi ndio wenye nchi na bunduki ni fahari yao. Yaani jamaa wana club zao za michezo ya kulenga shabaha; ni sawa na kufuta Simba na Yanga hapa; huwezi kueleweka na "wenye nchi" walio wengi.
 
Kwanini wanafunzi wanaruhusiwa kuingia na silaha darasani?
 
Uhalifu unatokea sehemu yoyote cshulen tu kikubwa wadhibit silaha
 
Republicans hawataki kabisa kushindwa kwenye swala la udhibiti wa silaha. Wako tayari kuzigeuza shule kuwa kama kambi za jeshi ili mradi wao waendelee kumiliki silaha
 
Kwani kuzipiga marufuku na kumilikisha waalimu ipi afadhali!?..
 
Isiwe Tanzania haswa na walimu wetu wanavyo ishi kwenye mazingira magumu.....! Utasikia shule imeandaa eneo la makaburi kuzikia wanafunzi
 
Trump kashaanza sarakasi. Mamwinyi wa kimarekeni, akinaTrump, wanazipenda bunduki nadhani kuliko wanavyompenda Mungu. Ni ngumu sana kufuta umiliki binafsi wa silaha US kwa sababu mamwinyi ndio wenye nchi na bunduki ni fahari yao. Yaani jamaa wana club zao za michezo ya kulenga shabaha; ni sawa na kufuta Simba na Yanga hapa; huwezi kueleweka na "wenye nchi" walio wengi.

Nimewavulia kofia NRA, hawa jamaa mwisho aseh!, hawasikii wala hawaelewi.
Wamekaa kimya na sasa ndo wanajitokeza, halafu ndo kwanza wana blame media..

"After a week of media silence following the school shooting in Florida, the National Rifle Association went on the offensive in its first public response to the massacre, pushing back against law enforcement officials, the media, gun-control advocates and the teenage survivors of the massacre who have pleaded for stricter gun laws.." WP
 
Hao jamaa bunduki ni fahari yao; ni alama na ishara ya heshima, ubabe, na uweza. Kufuta umiliki binafsi wa bunduki US kwa kizazi hiki tusahahu. Kuna vizee vilishuhudia WWII, ubaguzi, na vita vya hapa na pale bado vinaishi kwao bunduki ni zaidi ya "mungu".
 
Kwani kuzipiga marufuku na kumilikisha waalimu ipi afadhali!?..
Hiyo habari ya kumilikishwa walimu hakuitamka kwa bahati mbaya au kwa maana halisi ya maneno yenyewe aliyotumia bali ni indirect way ya kusema haiwezekani kufuta umiliki binafsi wa bunduki Marekani. Mwenye ufahamu na afahamu.
 
wanaweza pitisha sheria kuzizuia uraiani na mwalimu akapewa kama kifaa cha shule!..
 
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule kama lile lililowaua watu 17 wiki iliopita mjini Florida.

''Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja'', alisema. Bwana Trump alitoa pendekezo hilo huku manusura wa shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Februari wakimtaka kuhakikisha kwamba shambulio kama hilo halitokei tena.

Rais huyo wa Republican pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki. Manusura wengine wakati huohuo waliwataka wa bunge wa Florida kuweka udhibiti wa bunduki.

''Tutakuwa thabiti iwapo kutakuwa na ukaguzi mbali hali ya kiakili ya mtu anayetaka kumiliki bunduki''. Trump aliwaambia wanafunzi kutoka shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas wakati wa hafla hiyo iliorushwa hewani moja kwa moja katika ikulu ya Whitehouse.

''Haitakuwa maneno kama ilivyokuwa awali'', aliongezea. Rais huyo wa Marekani pia aliunga mkono pendekezo lililoungwa mkono na muungano wa wamiliki wa bunduki NRA .

Aliaahidi kuangazia kuhusu wito kwa walimu kupewa bunduki. ''Iwapo una mwalimu ambaye ana bunduki'', alisema ''anaweza kusitisha shambulizi lolote kwa haraka. Iwapo mwalimu angemiliki bunduki , ijapokuwa najua ni swala ambalo lingezua utata, wangepewa mafunzi maalum na wangesaidia pakubwa''.

''Kusingekuwa na uhuru wa kuingia katika shule na kuanza kufyatua risasi, kwa sababu washambuliaji wangekuwa waoga''.

Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.

Rais huyo wa Marekani alisikiliza malalamishi ya mabadiliko ya sheria za umiliki wa bunduki siku ya Jumatano kutoka kwa wanafunzi 40 , walimu na familia.

Baadhi ya wale waliohudhuria hafla hiyo ya saa moja waliunga mkono wazo la rais Trump kuwahami walimu.

Lakini Mark Barden ambaye mwanawe aliuawa katika shambulio la 2012 katika shule ya Sandy Hook Elementary School mjini Connecticut - anasema ''ongezeko la bunduki sio suluhu. Walimu wana majukumu zaidi kwa sasa kwa wao kuchukua jukumu jingine la kutumia nguvu ili kumuua mtu'', alisema.

BBC
Trump ni boya kweli kweli. Kwani mfyatua risasi huwa anajulikana kwamba sasa hivi anataka kufyatua? si huwa ni tukio la kushitukiza?? tena mfyatuaji akijua mwalimu ana siraha ndo anaanza naye. Huyu rais ni bwege kweli kweli
 
kama watu wanaweza kushambulia vituo vya polisi kwenye silaha za kutosha na askari wenye mafunzo atashindwa shuleni?
hata waalimu wakipewa na mtaani zikawepo bado sio suluhisho!!

Trump bwana!!
 
Back
Top Bottom