Nature
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 819
- 2,212
Msanii mchekeshaji raia wa Marekani mwanamama Cathy Griffin alieonekana live kupitia kipindi cha TV kinachorushwa na CNN akiwa ameshika kinyago kinachofanana kabisa na kichwa cha rais Trump huenda akashtakiwa kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya Uhuru wa habari.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 57 alionekana akiwa amebeba kinyago cha Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, Jambo ambalo limezua hasira miongoni mwa watu wengi wakiwemo wapinzani wa Trump nchini marekani.
Baada ya Tukio hilo Kituo cha TV cha CNN kilitangaza kumfukuza kazi msanii huyo na kukifuta kipindi chake mara moja
Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo rais Trump mwenyewe wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa familia za Wanajeshi na baadhi ya waandishi wa habari wa Marekani waliochinjwa na Kikundi cha kigaidi cha ISIS
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi wa Rais nchini marekani (Secret Service) imesema uchunguzi umekamilika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani Cathy Griffin.
Kathy Griffin holds up Donald Trump's decapitated head in new photo shoot