Marekani kuondoa wanadiplomasia wake wote Venezuela

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,560
9,416

Marekani itawaondoa wafanyakazi wake wote wa ubalozi waliobakia nchini Venezuela. Amesema hayo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kwa njia ya Twitter.
Waziri Pompeo ameeleza kuwa, Marekani inachukua hatua hiyo kwa sababu hali imezidi kuwa mbaya nchini Venezuela.

Pia amesema uwepo wa wafanyakazi hao wa ubalozi nchini Venezuela unazuia hatua ambazo utawala wa Marekani ungeweza kuchukua juu ya Venezuela.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alishavunja uhusiano wa kibalozi baina ya nchi yake na Marekani mnamo mwezi wa Januari baada ya Marekani kutangaza hatua ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido.
 
Hiyo kauli inaashiria Kuna kitu kibaya kinafuata hapo so Bwana mkubwa Maduro ajiandae saa yeyote na muda wowote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujuma inafuata soon

Siku Akina Mohamed Al baradei walipotakiwa waondoke Iraq Kwenye ukaguzi wao wa Silaha Za Maangamizi ndio Siku Iraq ilipoanza kushambuliwa Na Majeshi ya NATO wakati wa Saddam Hussein Al Tikrit
 
hawa jamaaa wanajiona wao ndo kila kitu dunia hii sasa hapa wanataka kwafanya nini wezao. Marekani dumisheni amani acheni visasi vitaharibu maelewano.
 
Naona mambo yashaiva,wanawatoa watu wao ili wasidhurike wakianza kuishambulia venezuela,
marekani washaanza kuvitarget vituo vya uzalisha umeme kwa kuvilipua kwa kutumia cyber attack, tangu juzi vituo kama vitano vimeshalipuliwa kwa style ya cyber attack,
kwasasa asilimia 95 ya venezuela ni giza,wagonjwa karibu 500 washakufa kwa kukosa huduma za kiafya zinazoendana na matumizi ya umeme mfano watoto njiti wanaowekwa kwenye mashine,
lengo la marekani kutumia mbinu hii ni kutaka wananchi warise dhidi ya maduro,
kwa marekani ,venezuela itakuwa ni shamba darasa,wakifanikiwa huko nchi inayofuata ni iran
 
"Bila Marekani, duniani ni mahala salama sana na pazuri sana kwa kuishi.
Marekani ikiwepo na nguvu zake, kuishi duniani ni sawa na kuishi nusu ya Jehanam" - The Technologist.
 
  • Thanks
Reactions: ibn
Back
Top Bottom