FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,885
- 43,774
Wanatumia Dollar bilioni 600 kila mwaka kwenye masuala ya kijeshi, hii ni sawa na T.shs Trillion 1,300. Ikumbukwe bajeti ya Tanzania halisi huwa ni kama Trillion 15 tu, kwahiyo bajeti ya jeshi lao kwa mwaka ni bajeti yetu ya miaka karibu 100! Sasa ni aibu na kutudhalilisha kwa nchi kutumia Trillion 1,300 kwenye jeshi kwa mwaka halafu eti anakunyanyasa na MCC development fund ya billion eti 600, masharti kibao, wakati anachezea pesa mara 3,000 ya hizo kwenye kuua binadamu wenzake!