Safari bado ndefu bongo hata uwe unajua nini hauwezi pata chance yakutumika unakaa na mautaalam yako mpaka basi, mfano mm nilitengeneza website hii Y.D.C.P mwaka 2006 nikiwa imepita miaka 3 tangu nitoke form 4, and nilipo maliza chuo tu nkatengeneza MWANZA | TANZANIA | Mwanza City Directory
na hii ilikuwa bonge la project coz niliweka mpaka navigator ya maeneo muhimu ya mwanza. Ila sasa unakutana na pingamizi la kimazingira unaingia fani ingine.
Tanzania watalaam wapo bana basi 2.
Mkuu website yako inaitwaje na mie niitembelee@3D
Unathani Tanzania inaweza kua taayari kama sisi wenyewe hatujawa tayari?---mi nahisi ni uzalendo kulishikia bendera hili. Myself nimeshaonesha mfano katika web yangu na manufaa nimeshayaona (sio kazi ya kutuoa time bila mafanikio kama wengi wanavyodhani).
Kwanza TZ hatuna mfumo wa kuvumbua vipaji vya IT kutoka wakiwa wadogo....
mzee congz,nimeguswa na creativity yako
Tatizo ni siasa nyingi nchi hii hawajaweka vipaumbele au kama vipo basi hawavifanyii kazi zaidi ya kukaaa maofisini na kula hela za wafadhili.Ni vijana wangapi wanao onyesha vipaji vyao katika technology ila hawapati support(Iko wapi DIT,Arusha tech ,etc).
Wenzetu nchi za jirani wako mbali katika haya maswala mfano uganda Uganda Linux User Group .naona na arusha nao wameanzisha group yao ALC | Arusha Linux Community so vitu kama hivi vikianzishwa kila mahali hata katika vyuo vinavyo fundisha ICT kuwepo na department ambayo wanafunzi wanaweza kuendeleza idea zao ingekua jambo la busara.ni mtazamo tu!!!
Kweli mkuu hapo ni changa moto....mimi nilishaskia jamaa anatengeneza helcopter hapo dar lkn sijui aliishia wapi sijui alikosa support. serikali ingemfadhiri naamini angetengeneza.