Mapenzi yananitesa: Mpenzi wangu anapenda sana kununa

Culture Me

JF-Expert Member
May 24, 2017
10,447
21,160
Guys,

Naandika post hii kwa uchungu na hasira juu ya huyu kipenzi cha mimi, daah anapenda sana kununa bila sababu yaani akiamua kua kisirani hadi naogopa.

Nipo nae for almost 5 years now, yuko poa kwa mambo mengine kasoro hapo tu, nimechunguza nimegundua kila mwezi lazima kisirani chake kipande, sasa sielewi nini shida jamani.

Siku moja tukiwa poa nikamuuliza kwanini anakua hivyo weeh akanibadilikia kua namsimanga sijui namuhisi ana kichaa duuh ikawa ugomvi moto.

Rafiki zetu wametuchoka maana akiwa hivyo hakuna mtu anamsikia na maneno machafu anatoa wote wananywea.

Leo sasa kanitolea moja hiyo, tangu asubuhi kaamka kanuna namsemesha anajibu mkato au hajibu kabisa, kula hataki nikaona ngoja nimpishe nikaenda dukani kwa jirani nakunywa soda taratibu kaja na kuanzisha vurumai eti nimemtelekeza bila chakula halafu mimi nakula huku daah aibu mtaani.

Nisaidieni waungwana shida inaweza kua nini?
 
Mtafutie daktari wa saikolojia aongee nae na kumwaga yote yanayomsumbua na kumpelekea kuwa hivyo

Hapo ndipo utapata mwanzo wa kupata utatuzi wa kinachojiri.
Shida nikimgusia juu ya hali hiyo anasema namuhisi yeye ni kichaaa sasa sijui nitumie mbinu gani kumkutanisha na huyo daktar... daah!
 
Sitachelea kusema anaanzisha visa kwa sababu kuna kipya kinyemi..
Hapo namkatalia maana simu yake ipo wazi kwangu na hajawahi kuonesha viashiria vyovyote vya cheating tatizo lake ni hilo tu, anasema nimvumilie.
 
Back
Top Bottom